UKRIANE-ULAYA-MSAADA

Ulaya yawatolea msaada raia wa Ukraine

Msaada aa kibinadamu umetolewa kwa wakimbizi wa ndani 900,000 na wakimbizi 600,000 kutoka Ukraine waliokimbilia nchi jirani. Hapa, katika kambi ya wakimbizi karibu na mji wa Donetsk, nchini Urusi.
Msaada aa kibinadamu umetolewa kwa wakimbizi wa ndani 900,000 na wakimbizi 600,000 kutoka Ukraine waliokimbilia nchi jirani. Hapa, katika kambi ya wakimbizi karibu na mji wa Donetsk, nchini Urusi. REUTERS/Alexander Demianchuk

Misaada ya kibinadamu kutoka Ulaya imeanza kuwasili nchi Ukraine kwa lengo la kuwahudumia wakimbizi wa ndani waliyoyakimbia mapigano kati ya jeshi na waasi. Sehemu ya kwanza ya misaada hio iliwasili Jumanne wiki hii katika mji wa Dnipropetrovsk.

Matangazo ya kibiashara

Ndege tatu zilitua kwa siku moja tu ya jana, ambapo ni tukio la aina yake kwa nchi ya Ukraine, na misaada ya aina mbalimbali hususan chakula na mahitaji mengine ya kimsingi vimeletwa kwa ajili ya kuwahudumia wakimbizi wa ndani laki tisa na wakimbizi laki sita waliolazimika kukimbilia nchi jirani.

Mapema wiki hii, Kamishna wa misaada ya kibinadamu alitangaza msaada wa ziada wa Uro milioni 15 kwa mwaka huu.

Hayo yakijiri wapiganaji wanaoiunga mkono serikali ya Urusi, mashariki mwa Ukraine wamesema wamewarudisha nyuma wanajeshi wa Ukraine katika wilaya mbili katika jimbo la Donetsk.

Mapigano kati ya wapiganaji hao na wanajeshi wa Ukraine yamekuwa yakiendelea kwa zaidi ya miezi mitano Mashariki mwa nchi hiyo na zaidi ya watu elfu tano wamepoteza maisha.

Wapiganaji hao wamesema lengo lao ni kudhibiti kikamilifu Mashariki mwa Ukraine, katika vita ambavyo mataifa ya magharibi yakiongozwa na Marekani yameendelea kuishtumu Urusi kuwaunga mkono wapiganaji hao kwa kuwapa fedha na silaha.