UKRAINE-MAPIGANO-USALAMA

Ukraine: Debaltsevo yakabiliwa na mapigano makali

Mpiganaji wa vikosi vinavyotaka kujitenga kwa eneo la mashariki la Ukraine karibu na mji wa Debaltsevo katika jimbo la Donetsk Januari 28 mwaka 2015.
Mpiganaji wa vikosi vinavyotaka kujitenga kwa eneo la mashariki la Ukraine karibu na mji wa Debaltsevo katika jimbo la Donetsk Januari 28 mwaka 2015. AFP PHOTO / MANU BRABO

Mapigano yanaendelea kushuhudiwa mashariki mwa Ukraine, hususan pembezoni mwa mji wa Debaltsevo, ambapo waasi wanaoungwa mkono na Urusi wanajaribu kuuzingira mji huo au kuushambulia.

Matangazo ya kibiashara

Watu wengi wameuawa na makumi waliojeruhiwa, ambao wamesafirishwa katika hospitali mbalimbali za mji wa Debaltsevo.

Kwa mujibu wa mwanahabari wa RFI nchini Ukraine, Sébastien Gobert, takribani wanajeshi 200 wamejeruhiwa na wengi wao wako katika hali ya maututi.

Wapiganaji wanaoungwa mkono na Urusi mashariki mwa Ukraine wamebaini kwamba wako tayari kuwahamasisha vijana laki moja kujiunga nao wakati huu Marekani pamoja na mkuu wa Jumuiya ya kujihami ya nchi za magharibi Nato, wakitarajia kutoa silaha kwa wanajeshi wa serikali ya Ukraine.

Hayo yanajiri wakati mapigano makali yemeendelea kati ya vikosi vya serikali na waasi hao wanapigania udhibiti wa eneo muhimu la usafiri la Debaltsev mashariki mwa Ukraine.

Milio ya risasi na milipuko ya mabomu ilisikika karibu na mji unaodhibitiwa na serikali ya Ukraine wa Debaltsevo, mji ulio muhimu na ulio karibu na miji miwili ya Donetsk na Luhansk, inayodhibitiwa na waasi wanaoiunga mkono Urusi.