VATICAN-PAPA-MAREKANI-JAMII-DINI

Papa Francis awataka viongozi wa Kanisa kuwa kioo cha jamii

Papa Francis atalihutubia Bunge la Congress la Marekani ifikapo septemba 24 mwaka 2015.
Papa Francis atalihutubia Bunge la Congress la Marekani ifikapo septemba 24 mwaka 2015. AFP/Gabriel Bouys

Taarifa iliyotolewa jana alhamisi na idara ya mambo ya nje Vatican imesema Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis, kwa mara ya kwanza, atalihutubia Bunge la Congress la Marekani ifikapo septemba 24 mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati papa Francis amewaandikia risala maaskofu na viongozi wa Kanisa Katoliki akiwataka kuachana na kashfa ya ulawiti inayowahusisha viongozi wa Kanisa.

Kiongozi huyo wa kanisa katoliki duniani amesisitiza kuwa hakuna nafasi katika Kanisa kwa watu wanaojihusisha na vitendo hivyo, hivyo haifai kuficha uchafu wa aina hiyo kwa sababu za aina yoyote ile.

Papa Francis amesema Kanisa linafanya kila jitihada kuwalinda watoto, na wana haki ya kuwa na uaminifu nao kwani Kanisa ni eneo salama.

Papa Francis amezitaka taasisi za kanisa kuboresha kanuni zilizowekwa tangu mwaka 2011 kufuatia risala iliotumwa na mtangulizi wake Benedicto wa 16.

Baadhi ya viongozi wa Kanisa walikua wakilaumia kwa kujihusisha na kashfa ya kulawiti watoto, na hali hiyo iliwahi kuzua taharuki kati ya kanisa katoliki na waumini wa Kanisa hilo.