UKRAINE-URUSI-UFARANSA-UJERUMANI-DIPLOMASIA-AMANI

Mkutano kuhusu mchakato wa amani Ukraine

François Hollande (kulia), Angela Merkel (kushoto) na Vladimir Putin (katikati), wakati wa mazungumzo yao kwa ajili ya mpango wa amani Ukraine, katika mji wa Moscow, tarehe 6 Februari mwaka 2015.
François Hollande (kulia), Angela Merkel (kushoto) na Vladimir Putin (katikati), wakati wa mazungumzo yao kwa ajili ya mpango wa amani Ukraine, katika mji wa Moscow, tarehe 6 Februari mwaka 2015. REUTERS/Maxim Zmeyev

Wakizungumza kwa simu, Angela Merkel, François Hollande, Petro Porochenko na Vladimir Putin, wametangaza Jumapili Februari 8 kufanyika kwa mkutano wa kilele katika mji wa Misk Jumatano wiki hii, miezi kadhaa baada ya mkutano uliyofanyika katika mji mkuu wa Belarusi.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii mpya, hata hivyo, bado ni tegemezi kwa maendeleo ya mazungumzo yanayofanyika kwa siri. " Haijawa sahihi bado" kuwa mkutano huu unaweza kufanyika kwa wakati uliopangwa, Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani ameeleza Jumatatu wiki hii.

Mchakato uliyoanzishwa hivi karibuni na kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, pamoja na rais wa Ufaransa, François Hollande umethibitisha kudorora kwa hali ya usalama nchini ukraine, lakini mazungumzo ambayo yameanzishwa hivi karibuni yanaweza kutafutia suluhu machafuko hayo.

Jumapili Februari 8, Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier alibaini kwamba majuma mawili au matatu yajayo yatagubikwa na maamuzi kwa mafaniko ya jitihada za Ufaransa na Ujerumani, huku akibaini kwamba mkutano wa Jumatano wiki hii bado haujathibitishwa.

Urusi kwa upande wake kupitia Waziri wa mambo ya kigeni, Sergei Lavrov alionyesha matumaini yake mwishoni mwa juma hili katika mji wa Munich, akibaini kwamba "maamuzi muhimu" yatachukuliwa katika mji wa Minsk.

Ukriane imethibitisha kwamba wanajeshi 1500 wa Urusi waliingia katika ardhi yake mwishoni mwa juma hili lililopita.

Marekani bado inashikilia msimamo wake wa kuipa silaha Ukraine kwa lengo la kukomesha machafuko yanayoendelea mashariki mwa nchi hiyo. Msimamo ambao unapingwa na rais wa Ufaransa François Hollande, na kansela wa Ujerumani, Angela Merkel.