YEMEN-ULAYA-MAREKANI-Mapigano-Siasa-Usalama

Balozi zafungwa kutokana na hali ya wasiwasi Yemen

Vikosi vya polisi vitoa ulinzi kwenye Ubalozi wa Marekani katika mji wa Sanaa, Februari 11, mwaka 2015, wakati ambapo Washington imetangaza kuwaondoa wafanyakazi wake.
Vikosi vya polisi vitoa ulinzi kwenye Ubalozi wa Marekani katika mji wa Sanaa, Februari 11, mwaka 2015, wakati ambapo Washington imetangaza kuwaondoa wafanyakazi wake. REUTERS/Khaled Abdullah

Balozi za nchi za magharibi zimefunga milango na kusitisha shughuli zao nchini Yemen. Washington imejitetea uamzi wake kwa “ kudorora kwa hali ya usalama katika mji wa Sanaa”.

Matangazo ya kibiashara

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imebaini kwamba wafanyakazi wake wametakiwa kuondoka katika ardhi ya Yemen, na wakati huu wamesafirishwa hadi nchi jirani.

Nchi zingine za mataifa ya magharibi, kama Ufaransa na uingereza, zimechukua uamzi huo wa kufunga balozi zao. Hali ya wasiwasi imeendelea kutanda katika nchi hiyo kati ya watu kutoka jamii za Wasuni na Washia.

Uamzi wa Marekani wa kuondoa wafanyakazi wake na kufunga ubalozi wake nchini Yemen huenda ukavuruga harakati za Marekani za kukabiliana dhidi ya Al Qaeda, ambayo imeendelea kujidhatiti katika nchi ya Yemen.

Al Qaeda katika eneo la Warabuni (Aqpa), lilitangaza hivi karibuni kujiunga na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu. Hali hiyo inaweza kutatiza harakati za Marekani dhidi ya kundi hilo.

Wanajihadi kutoka jamii ya Wasuni nchini Yemen wametangaza kwamba wataunda kikosi maalumu chini ya usimamizi wa kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu kitakacho pambana dhidi ya mahasimu wao.

Mahasimu hao ni jamii ya Washia ambao kwa sasa wanadhibiti sehemu kubwa ya nchi ya Yemen. Mataifa mengi ya Ulaya yameamua kufunga balozi zao. Nchi hizo ni pamoja na Uingereza, Ufaransa, ambayo imewataka raia wake kuondoka nchini Yemen katika muda muafaka.