UKRAINE-UFARANSA-UJERUMANi-URUSI-AMANI-USALAMA

Tahadhari na furaha baada ya makubaliano ya Minsk

Rais wa Urusi Vladimir Putin anakabiliwa na vikwazo iwapo atashindwa kuacha kuwasaidia waasi wanaotaka kujitenga kwa eneo la mashariki mwa Ukraine. Hayo ni baada ya viongozi wanaojaribu kutafutia suluhu machafuko yanayoendelea kushuhudiwa mashariki mwa Ukraine.

Rais wa Ukraine, Petro Poroshenko bado ana wasiwasi kuhusu hatma ya amani ya kudumu mashariki mwa Ukraine.
Rais wa Ukraine, Petro Poroshenko bado ana wasiwasi kuhusu hatma ya amani ya kudumu mashariki mwa Ukraine. AFP PHOTO / KIRILL KUDRYAVTSEV
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo rais wa Ukraine Petro Porochenko amebaini kwamba hana imani na mkataba huo, kutokana na mwenendo wa Urusi wa kujikubalisha jambo ambalo haitatekeleza.

" Hatutarajii utekelezaji rahisi wa mchakato", amesema rais wa Ukraine Petro Poroshenko saa chache baada ya hitimisho ya mkataba wa amani katika mji wa Minsk Alhamisi asubuhi wiki hii, baada ya mazungumzo yaliyodumu masaa 14.

Rais wa Urusi, Vladimir Putin alilazimika kukubali kutia saini kwenye makubaliano yaliyozitaka pande mbili husika kusitisha mapigano. Rais wa Ufaransa, François Hollande na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel walizungumzia katika mkutano huo wa Minsk kama wasuluhishi wa mazungumzo.

Kwa mujibu wa mwanahabari wa RFI, mjini Kiev, Régis Genté, Ukraine bado ina wasiwasi na mwenendo wa Urusi kutokana na kuendelea kuwasaidia waasi. Nakala ya mkataba huo kimsingi, inayosimamia kwenye mkataba wa kwanza wa Minsk, uliyotiliwa saini Septemba 5 mwaka 2014 haielezii kwa kina kuwa Moscow itaacha kuendelea kuhatarisha usalama wa Ukraine kwa kuwasaidi waasi wanaotaka kujitenga kwa eneo la mashariki la nchi hiyo, wakati ambapo wanajeshi na fedha hutoka Urusi, amesema Porochenko.

Lakini katika mji wa Kiev, raia wamepokea kwa shangwe mkataba huo, wakibaini kwamba hali mbaya zaidi ambayo ingelitokea nchini Ukraine, imeepukwa. Usitishwaji mapigano umepatikana na kilicho bora zaidi, Urusi haikulazimisha mgawanyiko wa taifa la Ukraine.

“ Muhimu zaidi ni kwamba mpango wa Putin umefeli”, amesema mtaalamu wa masuala ya siasa, Olexyi Harani. “ Wazo lake lilikuwa kuigawanya Ukraine katika nchi mbili. Wazo la Putin lilikua kuunda jamhuri mbili ziliyo uhuru. Mpango wa Putine ulikua kuighoofisha Ukraine”, ameendelea kusema Olexyi Haran.

Umoja wa Ulaya umetishia kuichukulia Urusi vikwazo iwapo itashindwa kutekeleza mkataba huo, hasa kushindwa kuacha kuwasaidia waasi wanaotaka kujitenga kwa eneo la mashariki mwa Ukraine.