UKRAINE-AMANI-MAPIGANO-USALAMA

Pande mbili zaheshimu mkataba wa usitishwaji vita

Makubaliano ya usitishwaji mapigano yametekelezwa usiku wa Jumamosi na Jumapili mashariki mwa Ukraine, lakini milio ya risasi na milipuko ya mabomu vimeendelea kusikika Jumapili Februari 15 katika mji wa Debaltseve.

Maelfu ya wanajeshi wa Ukraine wamepiga kambi karibu na mji muhimu wa Debaltseve.
Maelfu ya wanajeshi wa Ukraine wamepiga kambi karibu na mji muhimu wa Debaltseve. REUTERS/Gleb Garanich
Matangazo ya kibiashara

Wengi wamekua wakijiuliza huenda hali hiyo inayoukumba mji wa Debaltseve ndio chanzo cha ukosefu wa amani katika mji wa Donbass.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI, mashariki mwa Ukraine, Régis Genté, waasi wanotaka kujitenga kwa eneo hilo ambao wanaungwa mkono na Urusi, wanaonekana kuwa wako tayari kukubali lawama kwa kutokubali kupoteza mji wa Donbass. Debaltseve ni mkoa muhimu kwa waasi hao, kwani unaonyesha jinsi gani walivyoendelea kushikilia eneo la mashariki, lakini pia ni kwa sababu ni kituo muhimu cha reli.

Kauli za viongozi wa jimbo la Donbass ziko wazi. Alexandre Zakhartchenko, mkuu wa “eneo la Donetsk lililojitenga na Ukraine”, amethibitisha kwa mfano, makubaliano yaliyotiliwa saini katika mji wa Minsk, hayahusu mkoa wa Debaltseve. Ikimaanisha kuwa waasi hao wa naotaka kujitenga kwa eneo la mashariki mwa Ukraine wana haki ya kuendesha mashambulizi katika mji wa huo wa Debaltseve.

Wanajeshi kati ya 6000 na 8000 wanazingirwa na waasi hao katika mji wa Debaltseve.

Baada ya hatua hiyo usitishwaji mapigano, hatua nyingine inayofuata ni ubadilishanaji wafungwa kati ya jeshi la Ukraine na waasi wanaotaka kujitenga kwa eneo la mashariki.