UKRAINE-MAPIGANO-USALAMA

Mapigano yashuhudiwa ndani ya Debaltseve

Makubaliano yaliyoafikiwa katika mji wa Minsk wiki iliyopita hayajazaa matunda yoyote hususan kusitisha mapigano mashariki mwa Ukraine, kati ya jeshi la Ukraine na waasi wanaotaka kujitenga kwa eneo hilo la mashariki.

Gari ya kijeshi ya jeshi la Ukraine ikipigwa picha Jumanne, Februari 17 mwaka 2015 karibu na mji wa Debaltseve.
Gari ya kijeshi ya jeshi la Ukraine ikipigwa picha Jumanne, Februari 17 mwaka 2015 karibu na mji wa Debaltseve. REUTERS/Gleb Garanich
Matangazo ya kibiashara

Jumanne Februari 17, mapigano yameendelea kushuhudiwa katika mji wa Debaltseve, katika mkoa wa Donetsk. Maelfu ya wanajeshi wa Ukraine wamezingirwa katika mji huo muhimu mashariki mwa Ukraine.

Waangalizi wa jumuiya ya Usalama na Ushirikiano barani Ulaya (OSCE) wamekua wakijaribu kufika katika mji wa Debaltseve Jumanne wiki hii, wakati ambapo Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel alikuwa alitangaza baada ya mazungumzo kwa simu na marais wa Ufaransa na Ukraine Jumatatu wiki hii, kwamba viongozi wa Urusi na Ukraine walikua yalifikiana, kuwalindia usalama waangalizi hao, hususan kuwaruhusu kuingia mashariki mwa Ukraine.

Lakini kwa mara ya kwanza katika eneo hilo la mashariki mwa Ukraine, mapigano ya ana kwa ana yameshuhudiwa Jumanne Februari 17 katika mitaa ya mji wa Donbass kati ya wanajeshi na waasi wanaotaka kujitenga kwa eneo la mashariki mwa Ukraine.

Umoja wa Ulaya kwa upande wake, umetoa wito kwa pande zote husika kusitisha mapigano mara moja. Sharti kwa ajili ya kudumisha amani ambayo inaonekana ni suala tete kwa sasa.

Hata hivyo Urusi imeendelea kuzituhumu nchi za magharibi kuzuia mchakato wa amani nchini Ukraine. Mshauri wa masuala ya kidiplomasia nchini Urusi, Iouri Ouchakov amesema moja ya tishio kwa azimio la mgogoro ni vikwazo vya nchi za magharibi ziliyoiwekea Urusi, ambapo vikwazo vya mwisho vilianza kutekeleza tarehe 16 Februari. Kwa mujibu wa Ushakov, vikwazo hivi ni kinyume na sheria na vinarudisha nyuma maendeleo ya uhusiano kati ya Urusi na Umoja wa Ulaya.