UKRAINE-DEBALTSEVE-MVUTANO-USALAMA

Kati ya mvutano kuhusu hali inayojiri na mazungumzo ya kisiasa

Rais wa Ukraine Petro Prochenko (kushoto) na Johannes Hahn, Kamishna wa Umoja wa Ulaya wa Sera ya Ujirani na Mazungumzo, Februari 19 mwaka 2015 katika mji wa Kiev, Ukraine.
Rais wa Ukraine Petro Prochenko (kushoto) na Johannes Hahn, Kamishna wa Umoja wa Ulaya wa Sera ya Ujirani na Mazungumzo, Februari 19 mwaka 2015 katika mji wa Kiev, Ukraine. REUTERS/Valentyn Ogirenko

Mvutano umeendelea kushuhudiwa mashariki mwa Ukraine kati ya vikosi vya Ukraine na waasi wanaotaka kujitenga kwa eneo la mashariki mwa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Jumatano jioni wiki hii, rais wa Ukraine, Petro Porochenko, aliomba kutumwa kwa ujumbe wa askari polisi wa Umoja wa Ulaya chini ya kivuli cha Umoja wa Mataifa katika eneo la mashariki mwa Ukraine.

Viongozi wa Ulaya wanajaribu kutafuta msimamo wa pamoja ambao wanaweza kupitisha kwa kutafutia suluhu mogogoro kati ya pande hizi mbili.

Licha ya mji wa Debaltseve kuanguka mikononi mwa waasi, hali bado ni tete kwenye uwanja wa mapigano.

Rais wa Ukraine aliomba hivi karibuni Umoja wa Ulaya kutuma kikosi cha askari polisi ambacho kitahudumu chini ya kivuli cha Umoja wa Mataifa, na kitahusika na kufuatilia uheshimishwaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano mashariki mwa Ukraine. Makubaliano ambayo yalitiliwa saini juma lililopita katika mji wa Minsk. Lakini mpaka sasa ombi lake halijapatiwa jibu.

Zoezi la kuondoa silaha za kivita, moja ya makubaliano yaliyoafikiwa katika mji wa Minsk, haliwezi kufana, wakati ambapo vita vitakua bado havijasitishwa katika maeneo yote yanayokabiliwa na mapigano, ameonya Petro porochenko, ambaye hata hivyo, ameomba kuachiliwa huru kwa raia wa Ukraine ambao wamefanywa wafungwa na waasi, wakiwemo wale waliokamatwa hivi karibuni katika mji wa Debaltseve.