UKRAINE

Jeshi la Ukraine na waasi wabadilishana wafungwa

Vikosi vya Ukraine na waasi wanaoiunga mkono Urusi vimebadilishana wafungwa kadhaa katika mstari wa mbele mashariki mwa mji jana Jumamosi hiyo ikiwa ishara ya kwanza ya wazi katika maendeleo katika makubaliano ya kusitisha vita yaliyotiwa saini juma lililopita.

Huyu ni miongoni mwa wanajeshi waliobadilishana Jumamosi hii 21 Feb 2015
Huyu ni miongoni mwa wanajeshi waliobadilishana Jumamosi hii 21 Feb 2015 REUTERS/Gleb Garanich
Matangazo ya kibiashara

Ishara hiyo nadra ya matumaini imekuja kufuatia mashambulizi ya kukera ya waasi wanaoiunga mkono Urusi, katika eneo la mashariki, na kudhibiti mji kubwa kutoka kwa wafuasi na kuweka vitisho vya vikwazo vipya dhidi ya Moscow kutoka kwa waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani.

Waandishi wa habari wa AFP katika mji wa Zholobok wameshuhudia wanajeshi 139 wa Ukraine wakibadilishwa kwa waasi 52 Jumamosi usiku, katika mlinganyo nadra wa makubaliano yaliyo kiukwa kwa kiasiki kubwa ambayo yaliaanza kutekelezwa tarehe 15 Februari.

Baadhi ya wanajeshi walioachiwa walikuwa wamejeruhiwa na wachache walilazimika kutembelea magongo kwa umbali mrefu katika eneo la nchi hiyo lililoharibiwa kwa vita ya miezi kadhaa.