UKRAINE-URUSI-MAPIGANO-USALAMA

Amani bado ni ndoto mashariki mwa Ukraine

Hali ya usalama bado ni tete mashariki mwa Ukraine, licha ya kuwa milio ya risasi na milipiko vimepungua kwa kiasi fulani tangu siku za hivi karibuni.

Mwanajeshi wa Ukraine katika mji wa Artemivsk, katika jimbo la Donetsk, Februari 23 mwaka 2014.
Mwanajeshi wa Ukraine katika mji wa Artemivsk, katika jimbo la Donetsk, Februari 23 mwaka 2014. REUTERS/Gleb Garanich
Matangazo ya kibiashara

Jeshi na waasi, kila upande una nia ya kuendelea kushikila mji wa Marioupol pembezoni mwa bahari ya Azov.

Ni vigumu kwa sasa kujua iwapo usitishwaji wa mapigano katika eneo hilo la mashariki utatekelezwa vilivyo, wakati ambapo kila upande umekua ukienedelea kuongeza idadi ya wapiganaji wake karibu na mji wa Marioupol.

Zehemu mbili zimebaki zimebaki ni tatizo. Moja iko katika maeneo ya jirani ya Donetsk, ambapo mwanahabari wa RFI, Régis Genté, amesikia milipuko usiku wa Jumatatu Februari 23 kuamkia Jumanne Februari 24. Huenda lengo la waasi ni kuzishambulia ngome za jeshi ili waandelea kudhibiti eneo hilo kwa amani.

Tatizo lingine ambalo linata wasiwasi, linahusu maeneo ya pembezoni mwa bahari ya Azov. Waasi wanaotaka kujitenga kwa eneo la mashariki mwa Ukraine huenda wanapania kudhibiti bandari ya Marioupol. Serikali ya Ukraine imethibitisha kwamba ina taarifa kwamba zaidi ya magari ya kijeshi yalivuka hivi karibuni mpaka na Urusi na yalielekea katika mji wa Novoazovsk.