UGIRIKIULAYA-UCHUMI

Ugiriki: maudhui ya mageuzi yatolewa hadharani

Waziri mkuu wa Ugiriki, Alexis Tsipras.
Waziri mkuu wa Ugiriki, Alexis Tsipras. REUTERS/Alkis Konstantinidis

"Kulingana na mtazamo wa Tume ya Umoja wa Ulaya, orodha hii inatosha kwa kuandaa hatua muhimu kwa lengo la kuhitimisha tathmini yake".

Matangazo ya kibiashara

Huu ndio mtazamo wa kwanza rasmi katika mji wa Brussels baada ya kutangazwa Jumanne asubuhi wiki hii kupokelewa kwa orodha ya mageuzi na hatua ziliyotakiwa kutekelezwa Ijumaa wakati wa mkutano wa nchi zinazotumia sarafu ya Yuro, kwa kuongezwa muda wa miezi minne ya mpango wa msaada wa kifedha ambao unaendelea.

" Tumejikubalisha kupambana dhidi ya ukwepaji kodi na rushwa". Ni kwa maneno haya ya matumaini kutoka Tume ya Ulaya ambapo limeanza Jumanne Februari 24 asubuhi zoezi la kutathmini hatua iliyowasilishwa na Ugiriki kwa Tume ya Ulaya, Mfuko wa kimataifa wa Fedha pamoja na kwa miji mikuu ya nchini zinazotumia sarafu ya Ulaya.

Inabakia sasa kuona kama hatua hizi zitasahihishwa wakati wa mkutano wa nchi zinazotumia sarafu ya Yuro, ambao umepangwa kufanyika Jumanne Mchana Februari 24, amebaini mwandishi wa RFI, mjini Brussels, Pierre Benazet.

Ni lazima kusisitiza kwamba mashaka ambayo yalikuwepo mpaka dakika ya mwisho ya kuwasili kwa orodha hii kwa kiasi kikubwa kutokana na kwamba Athens Jumatatu wiki hii ilikutana na kushauriana na washirika wake wa Ulaya kwa kujihakikishia kuwa itapendekeza hatua kukubalika.