UTURUKI-IS-IRAQ-USALAMA

Ankara yaongeza nguvu katika vita dhidi ya IS

Jeshi la Iraq likiendesha mashambulizi katika mkoa wa Salaheddine kwa lengo la kuwatimua wapiganaji wa Islamic State.
Jeshi la Iraq likiendesha mashambulizi katika mkoa wa Salaheddine kwa lengo la kuwatimua wapiganaji wa Islamic State. REUTERS/Thaier Al-Sudani

Wanajeshi karibu 30,000 wa Iraq wameanzisha vita tangu siku mbili zilizopita kwa lengo la kudhibiti Tikrit, mji muhimu na wenye ishara, ambao unapatikana kilomita 160 kaskazini mwa Baghdad. Lakini kuendelea kwao katika mapigano hayo kutachukua muda kuliko ilivyokua ikitarajiwa.

Matangazo ya kibiashara

Kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu limeweka mabomu na vilipuzi mbalimbali kwenye barabara inayoelekea kwenye ngome zake. Katika operesheni hii, jeshi la Iraq linatumainia msaada kutoka Iran, ambayo imepeleka kamanda wa kikosi cha Qods, kitengo maalumu cha jeshi la Iran.

Msaada mwingine, ni ule wa Uturuki, ambayo ilipeleka ndege mbili za mizigo zinazobeba vifaa vya kijeshi nchini Iraq. Huu ni msaada muhimu kutoka Ankara.

Jumanne wiki hii, Uturuki ilitoa ishara za kwanza kwa kushiriki hadharani katika vita dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola al Kiislamu. Uturuki imepeleka ndege ya mizigo iliyobeba vifaa vya jeshi ili kulisaidia jeshi la Iraq linaloendesha vita dhidi ya wapiganji wa Dola la Kiislamu kwa lengo la kuudhibiti mji wa Tikrit.

Kwa mjibu wa mwandishi wa RFI, Istanbul, Jérôme Bastion, serikali ya Uturuki imemetangaza kutoa ushiriki wake siku za hivi karibuni katika vita vya kuuteka mji wa Mossoul.

Waziri wa ulinzi wa Uturuki, Ismet Yilmaz, amesema Uturuki ni moja ya nchi zinazounda muungano wa kimataifa unaoendesha vita dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu.

“ Haitowashangaza kuona Uturuki inaruhusu majeshi yake ya angani kushiriki katika muungano huo unaoongozwa na Marekani", amesema Yilmaz.

Kwa upande wake waziri mkuu wa Uturuki, Ahmet Davutoglu, amebaini kwamba usalama wa Mossoul ni moja ya majukumu ya Ankara.

“ Kundi la wapiganaji wa Doala la Kiisalamu ni tishio pia kwa Uturuki”, amesema waziri mkuu wa Uturuki, Ahmet Davutoglu,