MAREKANI-UKRAINE-URUSI-USALAMA

Obama aombwa kuipa silaha Ukraine

Wabunge wa Marekani wanamuomba rais Barack Obama kuipa silaha Ukraine.
Wabunge wa Marekani wanamuomba rais Barack Obama kuipa silaha Ukraine. REUTERS/Kevin Lamarque

Wabunge wa vyama vya Republican na Democratic nchini Marekani wanamhimiza rais Barrack Obama kuipa silaha Ukraine kupambana na waasi wanaoiunga mkono serikali ya Urusi.

Matangazo ya kibiashara

Wabunge hao wamemwandikia Barua Spika wa Bunge la Congress, John Boehner, na kusisitiza kuwa kitendo cha Urusi kuendelea kuwaunga mkono waasi kwa kuwapa silaha na fedha ni kinyume na sheria za Kimataifa.

Aidha, wabunge hao wanadai kuwa mkataba uliofikiwa hivi karibuni umeonekana kuwa faida kwa waasi ambao wanaendelea kudhibiti maeneo mengi Mashariki mwa Ukraine.

Urusi imekuwa ikikanusha nadai kuwa inawapa silaha waasi hao na pia kudokeza kuwa wanajeshi wake wanaopigana Mashariki mwa nchi hiyo ni wale wanaojitolea.

Rais Barrack Obama amekuwa akisema kuwa yuko tayari kuipa silaha serikali ya Ukraine ikiwa Urusi itaendelea kuwaunga mkono waasi wanaotaka kujitenga kwa eneo la Mashariki.

Watu zaidi ya elfu 6 wamepoteza maisha Mashariki mwa Ukraine tangu kuanza kwa vita mwaka uliyopita.