UFARANSA-ARGENTINA-AJALI-UCHUNGUZI-USALAMA

Argentina: wachunguzi wa BEA kwenye eneo la ajali

Wataalam wawili wa Ofisi ya Uchunguzi na Uchambuzi kutoka Ufaransa, BEA, wanatazamia kuanza uchambuzi wao kwenye mabaki ya helikopta Alhamisi wiki hii.
Wataalam wawili wa Ofisi ya Uchunguzi na Uchambuzi kutoka Ufaransa, BEA, wanatazamia kuanza uchambuzi wao kwenye mabaki ya helikopta Alhamisi wiki hii. REUTERS/Reuters TV

Jaji mpya ameanza kushughulikia kesi ya ajali ya helikopta iliyotokea Jumatatu wiki hii katika mkoa wa La Rioja, kaskazini mwa Argentina, ajali ambayo iligharimu maisha ya raia wanane wa Ufaransa.

Matangazo ya kibiashara

Wanamichezo Florence Arthaud, Camille Muffat na Alexis Vastine, ambao walikua wakishiriki katika utengenezaji wa makala ya " télé-réalité”, ni miongoni mwa waliofariki. Uchunguzi bado unaendelea ili kujua chanzo cha ajali hiyo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI, katika mji wa Buenos Aires, Jean-Louis Buchet , Jumatano asubuhi wiki hii, katika kijiji cha Villa Union, kijiji kiliyo karibu na eneo la ajali, jaji wa Mahakama kuu alikutana na jaji wa mkoa ambaye anaendelea na uchunguzi hadi sasa kwa kuiweka mikononi mwake kesi hiyo.

Kutokana na hali ya kesi ikiwa ni pamoja na ukweli kwamba raia wa kigeni waliangamia katika ajali hiyo, Mahakama kuu ya kitaifa ndio itashughulikia kesi hiyo. Ilichukua masaa 24 ili kuteua jaji wa Mahakama kuu ya kitaifa, na masaa 12 mengine kwa ajili ya jaji huyo kujielekeza kwenye eneo la ajali.

Baadae jaji huyo aliialika timu iliyokua ikijianda kutengeneza makala hayo, ambayo bado iko katika kijiji cha Villa Union, ili kueleza jinsi ilikua ikijianda kuendesha kazi yake. Jaji huyo ameiambia timu hiyo kwamba alikua anataka kuhoji baadhi ya watu, ikiwa ni pamoja na viongozi wa timu hiyo na mashahidi wa ajali. Orodha ilikua inatazamiwa kutolewa usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi wiki hii, ili mahojiano yaweze kuanza Alhamisi Machi 12.

Nia ya serikali ya Ufaransa ambayo inawasiliana na vyombo vya sheria vya Argentina nikutaka taratibu ziendeshwe kwa haraka iwezekanavyo ili timu hiyo inayohusika na kutengeneza makala kwenye runinga ya Ufaransa ya TF1 iweze kurejea Ufaransa siku zijazo.

Hata hivyo, wataalamu wa Ofisi ya Uchunguzi na uchambuzi kutoka Ufaransa, BEA, waliowasili Jumatano usiku wiki hii katika kijiji cha Villa Union, wataanzia kazi yao kwenye mabaki ya helikopta leo Alhamisi kwa ushirikiano na wachunguzi kutoka Argentina. Uchunguzi unaonekana kuwa mgumu, kinyume na kile ambacho jaji alisema awali, helikopta ndogo, ambazo hazina visanduku vyeusi vinavyorikodi matukio katika ndege.

Wataalamu hao wataendesha uchunguzi wao wakitumia taaluma waliyonayo kwenye mabaki ya helikopta na hivyo kukamilisha kazi yao. Ripoti ya wataalamu inatarajiwa kutolewa katikati ya wiki ijayo.