SWEDEN-UINGEREZA-ECUADOR-ASSANGE-SHERIA

Julian Assange atahojiwa London na majaji wa Sweden

Julian Assange akiwa katika  Ubalozi wa Ecuador mjini London tarehe 20 Desemba mwaka 2012.
Julian Assange akiwa katika Ubalozi wa Ecuador mjini London tarehe 20 Desemba mwaka 2012. REUTERS/Luke MacGregor/files

Julian assange amekubali kuhojiwa mjini London, kwa ombi la ofisi ya Mashtaka ya Sweden, ambayo inachunguza kwa kipindi cha miaka minne kuhusu tuhuma za ubakaji dhidi ya mwanzalishi wa WikiLeaks.

Matangazo ya kibiashara

Julian Assange anapewa hifadhi ya ukimbizi katika ubalozi wa Ecuador nchini Uingereza kwa kipindi karibu cha miaka mitatu sasa.

Kwa mujibu wa mwanasheria wake, raia kutoka Sweden, Per Samuelssonn, Julian Assange ni ” mwenye furaha na inatakiwa utaratibu wa sheria ufuatwe ili mteja wangu afutiwe makosa anayotuhumiwa”, amesema Per Samuelssonn.

Assange alikua akipendekeza jambo hilo tangu miaka minne iliyopita, lakini Ofisi ya Mashtaka ilikua ikitaka mahojiano yafanyike nchini Sweden kuhusu kesi hiyo. Miaka mingi ilipita tangu raia wawili wa Sweden walipofungua mashtaka ya ubakaji dhidi ya Assange, na ndani ya miezi sita vielelezo vitakusanywa. Ofisi ya Mashtaka itasubiri kwa sasa idhini kutoka Uingereza na Ecuador.

Julian Assange kwa sasa anapewa hifadhi ya ukimbizi katika ubalozi wa Ecuador mjini London tangu mwezi Juni mwaka 2012. Raia huyo wa Australia anakabiliwa na hati ya kukamatwa iliyotolewa na Mahakama ya Ulaya. Assange anasema hana hatia kuhusu tuhuma za ubakaji zinazomkabili, lakini anaogopa kuwa Sweden huenda ikamsafirisha hadi upande wa pili wa bahari ya Atlantiki.

Julian Assange anatafutwa na Marekani kutokana na kuchapishwa kwenye mtandao alioanzisha wa WikiLeaks, nyaya 250,00 za kidiplomasia za Marekani na ripoti 500,00 za kijeshi ambazo ziwekwa kama siri ya ulinzi.