VANUATU-KIMBUNGA PAM-JAMII

Vanuatu: mshikamano wa kimataifa waanza kutekelezwa baada ya kimbunga

Vanuatu, moja ya nchi maskini zaidi duniani, Kimbunga Pam kimeteketeza vijiji kadhaa katika kisiwa hiki.
Vanuatu, moja ya nchi maskini zaidi duniani, Kimbunga Pam kimeteketeza vijiji kadhaa katika kisiwa hiki. REUTERS/UNICEF Pacific/Handout via Reuters

Msaada wa kimataifa umeanza kuwasili katika kisiwa cha Vanuatu, ambacho kimekumbwa na kimbunga Pam Jumamosi Machi 14.

Matangazo ya kibiashara

Idadi ya watu walioathirika na kimbunga hiki, kinachoarifiwa kuwa moja ya majanga mabaya zaidi kutokea katika ukanda wa Pasifiki ya Kusini haijafahamika. kisiwa hiki chenye wakaazi 275,000, ni miongoni mwa nchi maskini zaidi duniani. Jumatatu wiki hii, rais Baldwin Lonsdale amesema kuwa mabadiliko ya hali ya hewa " yamechangia" kuipa nguvu dhoruba hiyo Pam.

Ufaransa imetuma ndege yake ya kijeshi aina ya Casa, ambayo iliruka ikitokea Nouméa, New Caledonia hadi Port Vila, mji mkuu wa Vanuatu, ikiwemo timu ndogo ya askari watatu, afisa wa usalama pamoja na afisa wa shirika la Msalaba Mwekundu.

Ufaransa imekua ikifanya tathmini ya mahitaji baada ya kimbunga hiki. Australia na New Zealand zimetuma ndege nne kwa minajili ya mahitaji muhimu ya raia. Ufaransa na nchi mbili kubwa katika kanda ya Pacific wana mikataba ya kuratibu uwezo wao wa msaada wakati kunapojitokeza janga katika kanda hiyo. Wafanyakazi wa idara mbalimbali za Ufaransa watatumia magari na vifaa vingine, huku wakisaidiwa na picha za satelaiti kwa kutafsiri kiwango cha mahitaji katika maeneo yaliyoathirika zaidi.

Kwa sasa hakuna kinachoendelea katika mji mkuu Port Vila na watu wanaonekana wakiwa wamesimama barabarani bila ya kupata msaada wowote na maelfu wamelazimika kulala nje baada ya maakazi yao kuharibiwa.

Rais Baldwin Lonsdale akizungumza katika mkutano wa Kimataifa nchini Japan siku ya Jumamosi, ameiomba Jumuiya ya Kimataifa kuisaidia nchi yake na kuwasaidia wananchi wake ambao wana mahitaji mengi kwa sasa.

Rais Lonsdale amesema ” nazungumza nanyi kwa moyo mzito sana, na sijui kimbuga hiki kitatuathiri hadi lini, nawaomba mtusaidie ili wananchi wetu wapate afueni.”
Tayari Umoja wa Mataifa, New Zealand, Australia na Uingereza zimeahidi kutoa kwa Kisiwa hicho kutokana na kimbuga hiki kibaya kuwahi kutokea katika nchi hiyo ndogo yenye zaidi ya watu Laki Mbili.

Mambo muhimu yanayohitajika kwa sasa katika kisiwa hicho ni ujenzi wa makazi ya watu waliokimbia makwao, maji safi ya kunywa pamoja na chakula.