MAREKANI-UFARANSA-USALAMA-MAZUNGUMZO-DIPLOMASIA

White House yatuliza utata juu ya kauli ya Kerry kuhusu Assad

John Kerry alithibitisha Jumapili kwamba " inatakiwa kumaliza mazungimzo" na Bashar al-Assad ili kusitisha machafuko ambayo yamegharimu maisha ya watu zaidi ya 215,000 kwa kipindi cha miaka minne.
John Kerry alithibitisha Jumapili kwamba " inatakiwa kumaliza mazungimzo" na Bashar al-Assad ili kusitisha machafuko ambayo yamegharimu maisha ya watu zaidi ya 215,000 kwa kipindi cha miaka minne. REUTERS/Brian Snyder

Kufuatia kauli ya John Kerry juu ya utawala wa Bashar al-Assad, ambaye alisema hivi karibuni kuwa " inatakiwa kumaliza mazungumzo", utata umeibuka katika mataifa mbalimbali.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya kauli hiyo ya kiongozi wa juu katika serikali ya Marekani, maoni mbalimbali yameanza kutolewa hususan nchini Ufaransa. Nchini Marekani, hata hivyo, kauli ya John Kerry imezua utata utata.

Kauli ya John Kerry imepelekea rais wa Syria mwenyewe kutoa msimamo wake. Bashar Al Assad ameomba kauli ya John Kerry ni ifuatwe na matendo. Jumuiya ya kimataifa imepigwa na mshangao kufuatia kauli hiyo, nchi nyingi zimelaani ufunguzi wa mazungumzo kati ya Washington na Damascus.

Ufaransa mpaka sasa umepinga mazungumzo ya aina yoyote na Bashar Al Assad. Kwa mujibu wa Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, kufufua ushirikiano na rais wa Syria, ni kulitolea zawadi kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu.

" Kwa vyovyote vile, Ufaransa ni nchi huru. Sera yetu ikilinganishwa na janga la kutisha linaloendelea kushuhudiwa nchini Syria haijabadilika. Sera hii inaendeshwa kwa amani na sheria za kimataifa", amesema Laurent Fabius.

Kwa upande wake, Waziri mkuu wa Ufaransa, Manuel Valls, amelani vikali kauli ya John Kerry, akibaini kwamba hakuna mazungumzo na utawala wa Bashar Al Assad ambayo yanaweza kufanyika.

“ Hakutakuwa na suluhu yoyote nchini Syria kama Assad atakua bado madarakani, na John Kerry anajua hivyo", amesema Manuel Valls.