UGIRIKI-ULAYA-UCHUMI

Mkutano wa kujadili ombi la Ugiriki Brussels

Waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsiprasakiwa pamoja na rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Jean-Claude Juncker.
Waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsiprasakiwa pamoja na rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Jean-Claude Juncker. REUTERS/Yves Herman

Waziri Mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras amewasihi viongozi wenzake wa Umoja wa Ulaya kuja na mbinu za kuisaidia nchi yake kujikwamua kiuchumi.

Matangazo ya kibiashara

Tsiprasi amesisitiza mbinu hizo ni pamoja na mabadiliko muhimu ya kisiasa na kuheshimu demokrasia pamoja na mikataba ya pamoja ili kuisaidia.

Mkutano huo ulikuwa wa kisiasa. ulipangwa katika dakika ya mwisho kwa ombi la Athens ambayo ina matumaini ya kupata karibu Euros bilioni mbilikutoka benki kuu ya Ulaya.

Benki za Ugiriki zimo mbioni kufilisika, bila msaada huo mpya, serikali ya Ugiriki haiwezi kuwa na uwezo wa kulipa madeni wadhamini wake kabla ya mwisho wa mwezi wa Machi.