UFARANSA-UGAIDI-IS

Sheria ya kwanza inayoipa uwezo Idara ya ujasusi ya Ufaransa

Kwa mujibu wa waziri mkuu wa Ufaransa, Manuel Valls, " tishio la kigaidi limekua katika ngazi isiyokuwa ya kawaida" na kupelekea sheria hii ifanye kazi yake muhimu..
Kwa mujibu wa waziri mkuu wa Ufaransa, Manuel Valls, " tishio la kigaidi limekua katika ngazi isiyokuwa ya kawaida" na kupelekea sheria hii ifanye kazi yake muhimu.. REUTERS/Philippe Wojazer

Waziri mkuu wa Ufaransa Manuel Valls amewasilisha Alhamisi wiki hii muswada wa sheria kuhusu ujasusia au upelelezi katika kikao cha baraza la mawaziri.

Matangazo ya kibiashara

Mwezi Julai mwaka 2014, rais wa Ufaransa François Hollande alitaka muswada huo wa sheria ujadiliwe haraka iwezekanavyo kwa kukabiliana na ugadi ambao umekithiri wakati huu.

Hii ni sheria ya kwanza inayosimamia shughuli za Idara ya ujasusi ya Ufaransa. Lakini baadhi ya watu wamelaani kuwa sheria hiyo inakuja kukandamiza uhuru wa mtu binafsi.

"Jukumu letu sio kuwatia uoga raia", amesema Manuel Valls. Lakini waziri mkuu wa Ufaransa amekumbusha pia kuwa " kwa muda wa miaka mitatu tulikua tukisema tukisisitiza kuwa tishio la kigaidi limekua katika ngazi isiyokuwa ya kawaida". Tishio, ambalo ametaja kuwa limesambaa karibu ulimwengu wote, huku likifanywa na kundi la watu waishio nchi za kigeni kama watu waliopo kwenye ardhi ya Ufaransa.

Ili kuunga mkono madai yake, Manuel Valls alikumbusha idadi ya raia wa Ufarasa ambao wameshajiunga na makundi ya kijihadi. Manuel Valls amesema raia 1900 wa Ufaransa walihusika katika makundi ya kusafirisha watu hadi kwenye maeneo ambapo wanajihadi wamekua wakiendesha harakati zao, 1450 wanaripotiwa kuwa nchini Syria na Iraq.

Waziri mkuu wa Ufaransa amebaini kwamba idadi ya raia wa Ufaransa waliojiunga na makundi ya kijihadi iliongezeka mara dufu ndani ya kipindi cha miezi 15.