UFARANSA-UJERUMANI-UHISPANIA-AJALI-USALAMA

Airbus A-320 yaanguka kusini mwa Ufaransa

Airbus A-320 ya shirika la Germanwings imeanguka kusini mwa Ufaransa.
Airbus A-320 ya shirika la Germanwings imeanguka kusini mwa Ufaransa. AFP PHOTO

Ndege hiyo yenye chapa A-320 ya shirika la ndege la Germanwings, ambayo imekua ikifanya misafara katika miji ya Barcelona na Düsseldorf imeanguka, Jumanne asubuhi wiki hii katika mkoa wa Barcelonette, katika milima inayojulikana kama “ Trois Evêchés”, nchini Ufaransa.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa hii imethibitishwa na mamlaka ya safari za ndege (DGAC). Ndege hiyo imekua ikibeba abiria 148.

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya Ufaransa, ndege hiyo imeanguka katika milima inayojulikana kama “ Trois Evêchés“. Mabaki ya ndege hiyo yamepatikana, wizara ya mambo ya ndani imetangaza.

Ndege hiyo imetangazwa katika hali ya hatari saa nne na dakika 47 saa za Ufaransa, karibu na mkoa wa Barcelonnette.

Ndege, hiyo ni mali ya kampuni ya Germanwings, kampuni tanzu ya Lufthansa, ambayo ilikua ikifanya safari katika mji wa Barcelona, Uhispania na mji wa Düsseldorf, Ujerumani, na imekua na abiria 142 pamoja na wafanyakazi 6 ikiwa ni pamoja na marubani wawili na wahudumu wanne.

Waziri wa mambo ya ndani Bernard Cazeneuve, anatazamiwa kujielekeza kwenye eneo la tukio, Waziri mkuu Manuel Valls ametangaza.