UFARANSA-UJERUMANI-UHISPANIA-AJALI-USALAMA

Ajali ya A320: mmoja wa marubani alikua alifungiwa nje ya chumba cha marubani

Helikopta ya Polisi ya Ufaransa ikipaa kwenye eneo la ajali karibu  milima ya Alps, Machi 25 mwaka 2015.
Helikopta ya Polisi ya Ufaransa ikipaa kwenye eneo la ajali karibu milima ya Alps, Machi 25 mwaka 2015. REUTERS/Emmanuel Foudrot

Kisanduku cheusi cha ndege ya shirika la ndege la ujerumani iliyopata ajali katika milima ya Alps kimeanza kutoa taarifa zake za mwanzo.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na sauti na maneno vilivyorekodiwa, mmoja wa marubani aliondoka katika chumba cha marubani na hakurejea tena katika chumba hicho mpaka wakati ndege ilipopata ajali. Kisanduku cha pili cheusi cha ndege hiyo bado kinatafutwa. Familia ya watu waliofariki katika ajali hiyo zinasubiriwa Alhamisi wiki hii kupokelewa katika eneo la ajali.

Mmoja wa marubani wawili wa Airbus A320 ya shirika la ndege la Germanwings iliyoanguka Jumanne Machi 24 ikiwa na watu 150 katika milima ya Alps, kusini mwa Ufaransa alikua alifungiwa nje ya chumba cha marubani wakati ndege hiyo ilipoanguka. Haya yanabainishwa na kifaa cha kisanduku cha kwanza cheusi kiliyopatikana, kifaa ambacho kilirekodia sauti na maneno kutoka katika chumba cha marubani “ Cockpit Voice Recorder” (CVR).

" Wakati ndege ilipokua ikipaa angani, marubani na wafanyakazi wengine katika ndege hiyo walikua wakiongea. Muda mchache baadae kulisikika sauti ya moja ya viti kikisogezwa nyuma, huku mlango ukifunguliwa na kufungwa, na baadae kulisikika fujo ya mtu ambaye alikua akigonga kwenye mlango. Wakati huo hakukuweko na mazungumzo tena hadi pale ndege ilipoanguka", kimebaini chanzo kilio karibu na uchunguzi, ambacho kilipata nafasi ya kusikia kumbukumbu hizi za sauti ziliyorekodiwa.

Haijulikani ni rubani gani ambaye alikua nje ya chumba cha marubani lakini wote walikua wakiongea kwa lugha ya Kijerumani.