Mvutano wajitokeza katika vyama vya mrengo wa kushoto Ufaransa

Martine Aubry na Manuel Valls, wakiwa katika mji wa Lille, wakati wa kampeni kwa uchaguzi wa serikali za mitaa, Machi 18 mwaka 2015.
Martine Aubry na Manuel Valls, wakiwa katika mji wa Lille, wakati wa kampeni kwa uchaguzi wa serikali za mitaa, Machi 18 mwaka 2015. REUTERS/Pascal Rossignol

Baada ya kushindwa katika uchaguzi wa mikoa, wafuasi wa chama cha kisochalisti wanatazamiwa kukutana.

Matangazo ya kibiashara

Serikali, Rais Hollande na Waziri Mkuu Manuel Valls, wanatazamiwa kukutana kwa mazungumzo na kundi la wafuasi wa chama cha Kisochalisti wanaotaka mabadiliko ya kisiasa yanayofuatishwa na chama cha Kisoshalisti.

François Hollande na Manuel Valls wamekua wakishinikizwa na kundi la wafuasi hao wa chama cha Kisoshalisti wanaotaka mabadiliko. Wawili hao , bila kusubiri mkutano uliopangwa kufanyika Jumatatu wiki hii, baada ya kutangazwa kushindwa katika uchaguzi wa mikoa, wametoa tangazo la pamoja la kuupa kipaombele " mkutano wa mkataba".

" Bila mabadiliko ya kweli katika siasa, bila kurekebisha upya utendaji kazi wa utawala, kusambaratika kwa mrengo wa kushoto hakutawezekana",  wameonya viongozi hao.

 Jumapili mwishoni mwa juma hili, waziri wa utamaduni kutoka chama cha Kisoshalisti, Aurélie Filipetti, ametoa wito kwa serikali kubadili sera yake, akibaini kwamba hakuna jinsi mtu kipofu anaweza kuendelea kuongoza kipofu. Waziri huyo amenyooshea kidole cha lawama timu iliyo madarakani, akibaini kwamba kushindwa katika uchaguzi huo kumesababishwa na timu hiyo.

" Wapiga kura wa mrengo wa kushoto hawakuhamasishwa vya kutosha, kwani wanaghadhibishwa na matokeo ya sera za serikali, kutokuepo na matokeo mazuri katika suala la uchumi, ambalo linapelekea siasa ya nchi kuporomoka”, amesema waziri Filipetti.

Chama cha UMP cha Nicolas Sarkozy kimeshinda uchaguzi huo wa mikoa.