UTURUKI-POLISI-SHAMBULIO-USALAMA

Makao makuu ya polisi yashambuliwa Uturuki

Makao makuu ya polisi, katika mji mkuu wa Uturuki Istanbul, yalizingirwa baada ya shambulio la Jumatano Aprili 1 mwaka 2015.
Makao makuu ya polisi, katika mji mkuu wa Uturuki Istanbul, yalizingirwa baada ya shambulio la Jumatano Aprili 1 mwaka 2015. REUTERS/Osman Orsal

Watu wenye silaha wameendesha shambulio Jumatano Alaasiri wiki hii dhidi ya makao makuu ya polisi katika mji mkuu wa Uturuki, Istambul.

Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo liliwajeruhi askari polisi wawili, wakati ambapo mawanamke mmoja ambaye ni miongoni mwa washambuliaji aliuawa.

Shambulio hilo linatokea siku moja baada ya kutekwa nyara kwa Mwendesha mashtaka katika ofisi ya Mashitaka.

Polisi iliingilia kati, lakini hata hivyo Mwendesha mashtaka huyo na watekaji nyara wawili waliuawa. Jumatano wiki hii watu kadhaa walikamatwa. Inaarifiwa kuwa watu hao wana uhusiano wa karibu na vuguvugu la mrengo wa kushoto ambalo linahusishwa katika mashambulizi hayo mawili.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI, Instanbul, Jérôme Bastion, kundi la watu wawili wenye silaha walijaribu kuingia Jumatano wiki hii saa kumi na mbili jioni katika makao makuu ya polisi, huku wakifyatua risasi kwa kuwatawanya askari polisi waliokua kwenye ulinzi. Mwanamke mmoja, ambaye ni miongoni mwa washambuliaji aliuawa wakati wakurushiana risasi katika ya kundi hilo na polisi. Mwanamke huyo alikua alivalia vilipuzi, lakini hakufaulu kuvilipua. Mshambuliaji mwengine alikamatwa baada ya kujeruhiwa wakati alipokua akijaribu kutimka. Wakati huohuo askari polisi wawili walijeruhiwa.

Uchunguzi uliendelea Jumatatu jioni wiki hii. Hata hivyo vuguvugu la mrengo wa kushoto la DHKP-C limenyooshea kidole kuhusika katika mashambulizi hayo mawili.

Katika tangazo lililorushwa katika tovuti Jumanne wiki hii wakati majengo ya vyombo vya sheria yalipovamiwa, vuguvugu hilo lilionya kwamba makao makuu ya polisi yatalipuliwa iwapo watekaji nyara watakua wameuawa.

Polisi imebaini kwamba shambulio hilo la siku ya Jumatano wiki hii liliandaliwa na kutekelezwa na watu watano.