UFARANSA-TV5 MONDE-UDUKUZI

Uchunguzi waanzishwa kuhusu udukuzi wa matangazo ya TV5 Monde

Kituo cha runinga TV5 Monde kimedukuliwa Jumatano jioni na kundi la watu" Hackers " wanaodai kuwa wanachama wa IS.
Kituo cha runinga TV5 Monde kimedukuliwa Jumatano jioni na kundi la watu" Hackers " wanaodai kuwa wanachama wa IS. REUTERS/Christian Hartmann

Kituo cha runinga cha TV5 Monde nchini Ufaransa, kimeshambuliwa tangu Jumatano wiki hii baada ya matangazo yake kudukuliwa.

Matangazo ya kibiashara

Kwa sasa kituo hicho kinaendelea na harakati za kurejesha matangazo katika vituo vyake kumi na moja, baada ya watu wanaodai kuwa ni wanachama wa kundi la wapiganaji wa Islamic State kudukua matangazo yake.

Mkurugenzi wa kituo hicho amesema kuwa tayari wameanza kurusha matangazo yao, ila tu ni vipindi vilivyorekodiwa awali kwa sababu hawajafanikiwa kutatua udukuzi huo.

Awali katika ukurasa wa kwanza wa mtandao wake kulikuwa na bango la kundi lililojiita kundi lililojitenga la mtandao likiwa na maandishi mimi ni wa kundi la Islamic state.

Wadukuzi hao pia wamechapisha nyaraka katika mtandao wa kijamii wa kituo hicho wakidai kuwa ni vitambulisho vya familia za wanajeshi wa Ufaransa wanaopambana na wapiganaji wa Islamic State.

Mwezi Januari mwaka 2015 mitandao ya kijamii ya wanamgambo hao iliyokua ikijulikana kwa jina la “ Cybercaliphate “ ilifaulu kudukua baadhi ya akaunti za CentCom, kituo cha uongozi wa kikanda wa wizara ya ulinzi ya Marekani, Pentagone, katika Mashariki ya Kati.

Matangazo ya TV5 Monde yamedukuliwa na kundi la watu wanaojiita “ Cybercaliphate “ ambao ni wanachama wa kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu.

Kwa saa kadhaa ukurasa wa YouTube wa chombo hiki cha wizara ya ulinzi wa Marekani kilikua kikirusha hewani filamu rasmi za Islamic State. Wakati huo huo, akaunti ya Twitter CentCom ilikua ikirusha hewani matangazo ya nyaraka ziliyowasilishwa kama siri, lakini wito wa mauaji kwa wanajeshi wa Marekani ambao majina yao yalitajwa, barua pepe na namba za simu. Mara baada tu, akaunti ya Twitter ya Newsweek ilidukuliwa kwa kurusha hewani propaganda ya Islamic State.