INDIA-UFARANSA-USHIRIKIANO

Ziara ya kwanza rasmi ya Narendra Modi Ufaransa

Waziri mkuu wa India Narendra Modi, Machi 27 katika mji wa New Dehli.
Waziri mkuu wa India Narendra Modi, Machi 27 katika mji wa New Dehli. Narendra Modi

Waziri mkuu wa India Narendra Modi atafanya ziara ya kikazi ya siku tatu nchini Ufaransa Alhamisi Aprili 9 mwaka 2015.

Matangazo ya kibiashara

Hii ni ziara yake ya kwanza barani Ulaya. Lengo la ziara hii ni kuendeleza India pamoja na ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili. Na baadae atajielekeza Ujerumani.

Hata kama kiongozi kutoka jamii ya Wahindu alipigwa marufuku kuingia barani Ulaya mwaka 2002, baada ya machafuko dhidi ya Waislamu katika jimbo la Gujarat, Narendra Modi anatazamiwa kupokelewa kwa shangwe na nderemo katika mji wa Paris. Waziri Mkuu wa India anatazamiwa kukutana na viongozi wa makampuni mbalimbali pamoja na kutembelea shirika la ndege la Airbus katika mji wa Toulouse ili kuwavutia wawekezaji wa Ufaransa.

Suala la mkataba wa kuiuza India ndege 126 za kivita za aina ya Rafale limekua kama gumzo kati ya nchi hizi mbili . Hata hivyo, suala hili halikupewa kipaumbele kwa safari ya Waziri mkuu wa India amesema Jean-Joseph Boillot, mshauri wa klabu ya kituo cha utafiti na utaalamu kuhusu uchumi wa dunia.

" Kwa kawaida mazungumzo kuhusu suala hili, ambalo limezungukwa na giza, yalitakiwa kusonga mbele. Ziara hii barani Ulaya ni moja ya sehemu ya ziara ya kimataifa Narendra Modi aliyoipanga tangu uchaguzi wake. Ufaransa ni moja ya nchi tano muhimu zaidi katika historia ya kujitegemea kwa India. Raia wa Ufaransa wametakiwa kutofananisha ziara ya Narendra Modia nchini Ufaransa, ambayo ni sehemu ya agenda yake ya kidiplomasia, na uuzaji wa ndege za kivita za aina ya Rafale, amesema Joseph Boillot.

Suala la ndege za kivita za aina ya Rafale lina ajenda yake. Mazungumzo ni kweli "yamekwama" kwa zaidi ya miaka mitatu. Ufaransa na India wanatafautiana kwa bei. Bei hiyo ilitoka kwa euro bilioni 11 hadi euro bilioni 18.3. Ufaransa inapaswa kutoa ndege 18 za kivita pamoja na funguo. Ndege nyingine 108 zitaunganishwa katika kiwanda cha Hindustan Aeronautics katika mji wa Bangalore. Kampuni ya Ufaransa Dassault inayotengeneza aina ya ndege hizo inaamini kwamba zoezi hilo la kuunganisha ndege nchini India litachukua muda mrefu, hivyo gharama kuongezeka.