UFARANSA-TV5 MONDE-IS-UDUKUZI

TV5 Monde : serikali yahamasisha vyombo vya habari

Mawaziri wa utamaduni na mwenye dhaman ya mabo ya ndani, Fleur Pellerin na Bernard Cazeneuve, Aprili 9 mwaka 2015, wakiongea na wakuu wa vyombo vya habari.
Mawaziri wa utamaduni na mwenye dhaman ya mabo ya ndani, Fleur Pellerin na Bernard Cazeneuve, Aprili 9 mwaka 2015, wakiongea na wakuu wa vyombo vya habari. AFP PHOTO / BERTRAND GUAY

Kituo cha runinga ya kimataifa ya Ufaransa TV5 Monde kimerejesha matangazo yake hewani Alhamisi wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Kundi la watu wa “ Cybercaliphate “ wanaodai kuwa wanachama wa kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu walidukua matangazo yake usiku wa Jumatano Arpili 8 mwaka 2015.

Mitambo ya TV5 Monde, mtandao wake, akaunti zake za Twitter na Facebook pia vimeshambuliwa. Ni kwa mara ya kwanza vyombo vya habari vya Ufaranda, kama runinga na redio kukumbwa na kisa kama hiki. Alhamisi wiki hii, waziri wa mambo ya ndani Bernard Cazeneuve na waziri mwenye dhamana ya utamaduni Fleur Pellerin waliwapokea kwa mazungumzo viongozi kadhaa wa redio na televisheni nchini Ufaransa.

Mkutano huu uliolenga kwa viongozi hao kuwa makini zaidi, uliwakutanisha viongozi wa zaidi ya vyombo vya habri ishirini, ikiwa ni pamoja Le Monde, France Media Monde, France Television, BFMTV na AFP. Ili tukio hili lisirejei tena, waziri wa utamaduni amewahimiza viongozi hao kuwa makini kila mara.

Waziri Fleur Pellerin amewataka pia waandishi kwenye magazeti yanayochapisha habari kwenye mitandao mbalimbali kuwa makini wanapokua wakitekeleza kazi yao.

Awali katika ukurasa wa kwanza wa mtandao wake kulikuwa na bango la kundi lililojiita kundi lililojitenga la mtandao likiwa na maandishi mimi ni wa kundi la Islamic state.

Wadukuzi hao pia walichapisha nyaraka katika mtandao wa kijamii wa kituo hicho wakidai kuwa ni vitambulisho vya familia za wanajeshi wa Ufaransa wanaopambana na wapiganaji wa Islamic State.

Mwezi Januari mwaka 2015 mitandao ya kijamii ya wanamgambo hao iliyokua ikijulikana kwa jina la “ Cybercaliphate “ ilifaulu kudukua baadhi ya akaunti za CentCom, kituo cha uongozi wa kikanda wa wizara ya ulinzi ya Marekani, Pentagone, katika Mashariki ya Kati.

Matangazo ya TV5 Monde yamedukuliwa na kundi la watu wanaojiita “ Cybercaliphate “ ambao ni wanachama wa kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu.

Kwa saa kadhaa ukurasa wa YouTube wa chombo hiki cha wizara ya ulinzi wa Marekani kilikua kikirusha hewani filamu rasmi za Islamic State. Wakati huo huo, akaunti ya Twitter ya CentCom ilikua ikirusha hewani matangazo ya nyaraka ziliyowasilishwa kama siri, lakini wito wa mauaji kwa wanajeshi wa Marekani ambao majina yao yalitajwa, barua pepe na namba za simu. Mara baada tu, akaunti ya Twitter ya Newsweek ilidukuliwa kwa kurusha hewani propaganda ya Islamic State.