MAKEDONIA-UPINZANI-SIASA

Rais wa Makedonia atakiwa kuondoka madarakani

Moja kati ya waandamanaji katika maandamanao yaliitishwa na upinzani Makedonia, Jumapili 17 mwaka 2015.
Moja kati ya waandamanaji katika maandamanao yaliitishwa na upinzani Makedonia, Jumapili 17 mwaka 2015. REUTERS/Ognen Teofilovski

Mvutano unaendelea kati ya serikali na upinzani nchini Makedonia. zaidi ya watu 50,000 waliitikia wito wa upinzani wa kuandamana Jumapili Mei 17 katika mitaa ya Skopje.

Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya mahema mia moja yaljengwa mbele ya makao makuu ya Serikali ya Makedonia. Wakiitikia wito wa upinzani, zaidi ya watu mia moja wamepania kupiga kambi katika eneo hilo hadi kuangushwa kwa serikali ya Nikola Gruevski.

Jumapili Mei 17, zaidi ya watu 50 000 waliitikia wito wa upinzani wa kufanya maandamano makubwa zaidi katika historia ya nchi hiyo. Baada ya maandamano, hali ya wasiwasi imeendelea kutanda. Wawakilishi wa upinzani na serikali wanakutana Jumatatu wiki hii mjini Brussels kwa ajili ya mazungumzo chini ya mwamvuli wa Umoja wa Ulaya.

Hata kama ametengwa kitaifa na kimataifa, Nikola Gruevski amesema hatoachia madaraka. Wakati huo huo rais huyo ametolea wito wafuasi wake kumiminika mitaani Juamatatu jioni wiki hii, huku kukiwa na hofu kuwa huenda kukatokea makabiliano makali kati ya wafuasi wa rais Nikola Gruevski na wafuasi wa vyama vya upinzani.

“ Tunafahamu kwamba hataondoka mara moja, lakini tuko tayari kubaki katika eneo hili kwa muda mrefu kwa ajili ya kutetea demokrasia”, amesema Goce, moja kati ya wanafunzi waliyokua wakiandamana.

Jumapili mchana mwishoni mwa juma hili, kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo, waandamanaji walibebelea bendera za Makedonia na Albania, ikiwa ni ishara ya kukanusha kutokea kwa machafuko ya makabila.