UINGEREZA-MALKIA-EU

Hotuba ya Malkia nchini Uingereza yasubiriwa

Malkia Elizabeth II na Waziri Mkuu David Cameron katika Downing Street, London.
Malkia Elizabeth II na Waziri Mkuu David Cameron katika Downing Street, London. REUTERS/Stefan Wermuth

Nchini Uingereza, Malkia Elizabeth II anatazamiwa kutoa hotuba yake ya jadi leo Jumatano kuwasilisha mpango wa bunge wa serikali mpya. Hotuba ya Malkia inafuata itifaki isiyobadilika tangu mwishoni mwa karne ya kumi na tisa. Hotuba hii itatolewa katika ukumbi wa jengo la Bunge la Uingereza, lakini si Malkia ambaye ameiandika.

Matangazo ya kibiashara

Hotuba ya Malkia Elisabeth itagubikwa na masuala muhimu ikiwa ni pamoja na maandamalizi ya kura ya maoni kuhusu kubaki au la kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya kabla ya mwaka 2017. Ilikuwa suala muhimu kwa kampeni iliyoendeshwa na kiongozi wa serikali ya kihafidhina David Cameron.

David Cameron anatazamiwa kuchukua madaraka mara tu baada ya hotuba ya Malkia ili kujaribu kuwashawishi washirika wake wa Ulaya kukubali mabadiliko ya mkataba ya Umoja wa Ulaya.

Kurejesha nchini Uingereza baadhi ya taasisi za Umoja wa Ulaya na kuongeza masharti ya upatikanaji wa msaada wa kijamii kwa ajili ya raia kutoka nchi wanachama wa Umoja huo, hasa wale kutoka chi za mashariki. Kiwango hiki ndicho David Cameron anatarajia kupata ili kuweza kutetea kubaki kwa nchi yake katika Umoja wa Ulaya, na hayo ndiyo yamekua yakipendekezwa na wafanyabiashara wa Uingereza.

Pia inatarajiwa kwa hotuba ya malkia, kupunguza kodi kwa wafanyakazi maskini. Lakini wakati huo huo, ongezeko la VAT ifikapo mwaka 2020. Hatua nyingine zitatangazwa kama kuongeza masharti ya haki ya kugoma, fedha za ziada kwa ajili ya mfumo wa afya, ifikapo mwaka 2020, na suala jingine muhimu, kuongeza sheria za kupambana dhidi ya itikadi kali. Kwa mfano, kuchukuliwa kwa hatua ya kufungwa kwa baadhi ya misikiti inayoendesha shughuli zinazotajwa kuwa zenye msimamo mkali.