UFARANSA-YEMEN-NYARA-USALAMA

Yemen: video ya mateka wa Ufaransa yarushwa hewani

Maandamano ya kuomba kuachiliwa huru kwa Isabelle Prime, Sanaa, Machi 9 mwaka 2015.
Maandamano ya kuomba kuachiliwa huru kwa Isabelle Prime, Sanaa, Machi 9 mwaka 2015. AFP / MOHAMMED HUWAIS

Video ambayo ameonekana mateka wa Ufaransa Isabelle Prime imerushwa hewani Jumatatu wiki hii. Isabelle Prime alitekwa nyara Februari 24 mwaka huu katika mji mkuu wa Yemen, Sanaa.

Matangazo ya kibiashara

Video hiyo imethibitishwa na wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa, ambayo imehakikisha kwamba idara zote za serikali " zimesimama kidete " kuhakikisha kuwa mateka huyo anachiliwa huru.

Katika video hiyo ya sekunde ishirini na moja, Isabelle Prime ameonekana akivalia nguo nyeusi, huku akiikaa sakafuni, na akiwaomba marais wa Ufaransa François Hollande na wa Yemen Abd Rabbo Mansour Hadi, msaada ili aweze kuachiliwa huru. "Tafadhali mnisafirishe Ufarnsa haraka iwezekanavyo ”, amesema mateka huyo.

“ Hii ni video ambamo ameonekana Isabelle Prime ”, naibu msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa Alexandre Giorgini amesema, akithibitisha uhalali wa video hiyo, ambayo Rfi hakipendelea kuirusha hewani kwenye tovuti yake.

“ Idara zote za serikali ambazo zina uwezo zimesimama kwa pamoja ili kuhakikisha kuwa raia huyo wa Ufaransa na mkalimani wake wanaachiliwa huru “, amesema Alexandre Giorgini,

Rais wa Ufaransa aliomba kuachiliwa huru kwa mateka huyo baada ya kutekwa nyara Februari 24 katika mji wa Sanaa. Ni kwa mara ya kwanza picha za mateka huyo zinawekwa hadharani tangu kutekwa kwake nyara.

 

 

Isabelle Prime mwenye umri wa miaka 30, alitekwa nyara akijielekeza kazini kwake, akiwa ameambatana na mkalimani wake Chérine Makkaoui. Watu waliohusika na kisa hicho walikua walijificha nyuso zao.