UGIRIKI-ULAYA-UCHUMI

Ugiriki: Waziri wa fedha, Yanis Varoufakis, ajiuzulu

Yanis Varoufakis, amejiuzulu kwenye wadhifa wake wa waziri wa fedha wa Ugiriki, Jumatatu Julaia 6 mwaka 2015.
Yanis Varoufakis, amejiuzulu kwenye wadhifa wake wa waziri wa fedha wa Ugiriki, Jumatatu Julaia 6 mwaka 2015. REUTERS/Yves Herman

Waziri wa fedha wa Ugiriki, Yanis Varoufakis, amejiuzulu licha ya ushindi wa kura ya "hapana" katika kura ya maoni iliyofanyika Jumapili Jualai 5 nchini Ugiriki.

Matangazo ya kibiashara

Varoufakis ametetea uamzi wake wa kujiuzuluakinaini kwamba ni kwa nia ya kuwezesha kupata makubaliano na wakopeshaji wa nchi ya Ugiriki, akitoa mfano wa "upendeleo fulani wa baadhi ya wanachama wa eneo la chi zinazotumia sarafu ya Euro na wafadhili kwa kukosekana (kwake) katika mikutano."

" Nafikiria kama wajibu wangu wa kumsaidia Alexis Tsipras kuutumia vizuri, kwa utaratibu anaofikiria bora, mtaji tuliopewa na raia wa Ugiriki pamoja na maoni kura ya maoni ya jana Jumapili ", ameandika Yanis Varoufakis kwenye blog yake Jumatatu wiki hii.

 Kwa mujibu wa waziri huyo wa Ugiriki mwenye dhamana ya fedha, uwepo wake umekuwa kikwazo kwa harakati za mazungumzo yoyote kati ya Athens na wakopeshaji wake.

" Muda mfupi baada ya kutangazwa kwa matokeo ya kura ya maoni, nilipewa taarifa ya upendeleo fulani niliyotuhumiwa na baadhi ya wanachama wa kundi la nchi zinazotumia sarafu ya euro pamoja na " washirika" wakiwa pamoja [...] kwa ajili ya "kukosekana kwangu " katika mikutano , fikra ambyo waziri mkuu amesema kuwa ni kwa manufaa ya kupata makubaliano. Kwa sababu hiyo mimi naamua leo kujiuzulu kwenye wadhifa wa Wizari wa fedha ", amesema Yanis Varoufakis.

Varoufakis anajiuzulu siku moja baada ya ushindi usiiopingika wa kura ya "hapana" kwa hatua mpya ilioombwa na wakopeshaji wa Ugiriki, ikiwa ni pamoja na Tume ya Ulaya, Shirika la Fedha Duniani (IMF) na Benki Kuu ya Ulaya.

Kwa mtaalamu wa masuala ya mchumi Colletis Gabriel, ambaye amehojiwa na Frédéric Rivière wa RFI wakati wa kutangazwa kujiuzulu kwa Yanis Varoufakis, kuna "ishara ya mizani" ambayo imewasilishwa mara moja kwa wakopeshaji, lakini pia kwa sehemu ya chama cha Waziri mkuu Yanis Varoufakis, Syriza.