UGIRIKI-ULAYA-UCHUMI

Ugiriki yaahidi kufanya mageuzi ya kodi na pensheni

Euclid Tsakalotos, waziri mpya wa fedha wa Ugiriki, amewajibika kwa ajili ya kufanya ombi la misaada kwa kipindi cha miaka mitatu kulingana na utaratibu wa kukabiliana na mdororo wa uchumi unaotumiwa Ulaya.
Euclid Tsakalotos, waziri mpya wa fedha wa Ugiriki, amewajibika kwa ajili ya kufanya ombi la misaada kwa kipindi cha miaka mitatu kulingana na utaratibu wa kukabiliana na mdororo wa uchumi unaotumiwa Ulaya. REUTERS/Alkis Konstantinidis

Ugiriki imeahidi Jumatano Julai 8 mageuzi ya kodi na pensheni " tangu wiki ijayo" kwa ajili ya kupewa mkopo kwa kipindi cha miaka mitatu kulingana na utaratibu wa kukabiliana na mdororo wa uchumi unaotumiwa Ulaya, amesema waziri mpya wa fedha wa Ugiriki Euclid Tsakolotos.

Matangazo ya kibiashara

Katika barua aliyomtumia rais wa Braza la Ulaya, waziri mpya wa fedha wa Ugiriki, Euclid Tsakolotos, ameomba rasmi mkopo wa miaka mitatu, huku akijikubalisha kufanya mageuzi na hatua ambazo zinapaswa kuhakikisha utulivu wa fedha za umma (...)." Amependekeza "utekelezaji wa haraka, tangu wiki ijayo, wa hatua thabiti kwa ajili ya kurekebisha sekta ya kodi na pensheni.

Kwa upande wake Waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras amesema serikali yake iko mbioni kuandika mapendekezo mapya yatakayo kwamua mazungumzo ya kutafutia ufumbuzi wa matatizo yake ya kiuchumi.

Waziri Mkuu Manuel Valls ameonya dhidi ya "mpasuko" wa Ulaya iwapo Ugiriki itaondoka kutoka Umoja wa Ulaya, Julai 8, mwaka 2015, Bungeni.
Waziri Mkuu Manuel Valls ameonya dhidi ya "mpasuko" wa Ulaya iwapo Ugiriki itaondoka kutoka Umoja wa Ulaya, Julai 8, mwaka 2015, Bungeni. REUTERS/Jacky Naegelen

Hii inafuatia muda wa siku tano uliotolewa na viongozi wa Ukanda wa Ulaya mjini Brussels kwa nchi hiyo kuleta mapendekezo yake.

Kauli hii ya waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras inafuatia tamko la rais wa Baraza la Ulaya Donuld Tusk kwa bunge la Ulaya.

Bwana Tusk ameonya kuwa zimesalia siku tano tu za kutatua mgogoro wa Ugiriki la sivyo mambo hali itazidi kuwa mbaya.

Akizungumza wakati wa mkutano na viongozi wa ukanda wa Ulaya, Tusk amesema kuwa huu ndio wakati mgumu zaidi kwa bara ulaya.

Ugiriki imepewa hadi Ijumaa , siku ya mwisho ya kuwasilisha mapendekezo yake ya kukwamua uchumi wake.

Bwana Tusk ameitisha kikao kamili cha muungano huo mwishoni mwa wiki akisema kuwa iwapo Ugiriki itaishia kufilisika, basi hatua hiyo itakuwa na athari kubwa kwa Ukanda mzima wa Ulaya.

Hata hivyo rais wa tume ya Ulaya Jean-Claude Juncker, ameonya kuwa wameandaa mpango mbadala iwapo Ugiriki itaondoka kutoka kwa Umoja wa Ulaya.

Hayo yakijiri serikali ya Ugiriki imesema Benki zitaendelea kufungwa hadi siku ya Jumatatu.

Hatua hii inakuja, huku serikali ikisisitiza kuwa mtu anaweza kutoa Euro 60 kwa siku.

Kufungwa kwa Benki hizo kuliamualiwa tarehe 28 mwezi ujao kutokana na mzozo wa kulipa deni linaloikabili.

Benki za Umoja wa Ulaya nazo zimesema zinasitisha msaada kwa Benki za Ugiriki hadi pale serikali itakapotoa mapendekezo ya namna ya kulipa deni linaloikabili.

Waziri Mkuu Alexis Tsipras amewaambua wabunge wa Umoja wa Ulaya Jumatano wiki hii kuwa serikali itapendekeza mapendekezo mapya kwa wakopeshaji wa kimataifa kufikia leo Alhamisi.

Siku ya Jumapili viongozi wa Umoja wa Ulaya watakutana jijini Brussels kujadiliana mzozo wa kiuchumi nchini Ugiriki.