UGIRIKI-ULAYA-UCHUMI

Ugiriki: Alexis Tsipras atazamiwa kuchukua maamuzi

Alexis Tsipras mbele ya Bunge la Ugiriki Jumamosi Julai 11. Bunge linatakiwa kupitisha mpango wa kwanza wa mageuzi kabla ya Alhamisi Julai 16.
Alexis Tsipras mbele ya Bunge la Ugiriki Jumamosi Julai 11. Bunge linatakiwa kupitisha mpango wa kwanza wa mageuzi kabla ya Alhamisi Julai 16. REUTERS/Alkis Konstantinidis

Bunge la Ugiriki linatazamiwa kupitisha kabla ya Alhamisi wiki hii muswada wa kwanza juu ya mageuzi yaliyotolewa na wakopeshaji wa Ugiriki ikiwa ni pamoja na hatua mpya kali.

Matangazo ya kibiashara

Waziri mkuu Ugiriki Alexis Tsipras amejikubalisha kufanya haraka ili kupata idhni ya Bunge. hata hivyo vikwazo vya ndani ni vingii, katika chama chake na serikali yake, bila kusahau malalamiko ya baadhi ya raia.

Alexis Tsipras anatazamiwa leo Jumatano, kuanza mchakato huo haraka iwezekanavyo kwa muda wa siku tano. Baada ya uthibitisho wa mapendekezo ya mageuzi na Bunge la Ugiriki Jumamosi mwishoni mwa juma lililopita saa kumi za majira ya alfajiri, masaa 17 ya mazungumzo mjini Brussels na marais wa nchi zinazotumia sarafu ya Euro kati ya Jumapili na Jumatatu, kamati mbalimbali za Bunge zitajifunza mageuzi kati ya saa nne na saa kumi na mbili. Kisha Alexis Tsipras atakutana na viongozi wa chama kabla ya kuanza kwa kikao kitakacho wajumuisha wajumbe mbalimbali wa chama hicho tawala. Na huenda kikao hiki kikafanyika usiku wa manane Jumatano wiki hii.

Katika mahojiano ya zaidi ya saa moja, Alexis Tsipras alirejelea jinsi mazungumzo yalivyofanyika. Aliamua kuchukua changamoto ya kutetea mkataba huu mbele ya wabunge. " Wakati huo, nachukua jukumu kamili kwa makosa yangu na makosa yangu ya kuchukua uamzi, alikiri. Nilichukua jukumu la kutia saini kwenye nakala ambayo sikua na imani nayo, lakini nimelazimishwa kutekeleza. Sintokimbia majukumu yangu. Wakati huu, kilicho muhimu ni kuhakikisha kuwa nchi na na raia waenye pato la chini kuepuka janga kubwa, dororo wa kifedha, ambapo mfumo wa benki usinguki na wananchi wasipotezi akiba zao, na nchi isiendelei kudidimia ", amesema Tsipras.

Katika mji wa Athens, wabunge wengi wanadhani kwamba Alexis Tsipras atafanya mageuzi ya serikali Alhamisi wiki hii, akiwaachisha kazi mawaziri ambao hawakupigia kura mageuzi hayo. Lakini kwa sasa, Waziri Mkuu wa Ugiriki amefuta uchaguzi wa haraka. " Nataka kuhakikisha kwamba chaguo ambao ntafanya chini ya shinikizo liweze kutekelezwa. Sina sababu ya kutaka uchaguzi, alielezea katika mahojiano yake. Kila kitu kitategemeakwa kile kitakachotokea katika siku zijazo ", ameongeza Tsipras.

Euro bilioni 312 zatakiwa kulipwa

Kama kila kitu kitakwenda kama ilivyopangwa, basi Ugiriki uitaweza kuanza mazungumzo kwa ajili ya kupata mpango wa tatu wa msaada wa zaidi ya Euro bilioni 80 ili kuiwezesha kulipa wakopeshaji wake. Kwa sababu Athens inakabiliwa na mzigo wa madeni ambayo inatazamiwa kuanza kulipa wiki ijayo. Baada ya kushindwa kulilipa Shirika la Fedha Duniani tarehe 30 Juni, Ugiriki imeendelea kukabiliwa na mzigo wa madeni. Nchi hii imeshindwa pia kulilipa shirika hilo Jumatatu wiki hii takriban Euro milioni 450.