UGIRIKI-ULAYA-UCHUMI

Bunge la Ugiriki lapitisha awamu ya pili ya mageuzi

Waziri mkuu Alexis Tsipras hakuwa na njia nyingje ispokua kuwashawishi wabunge wa Ugiriki kupigia kura mfuko wa pili wa hatua kali za malipo ziliyotolewa na wakopeshaji.
Waziri mkuu Alexis Tsipras hakuwa na njia nyingje ispokua kuwashawishi wabunge wa Ugiriki kupigia kura mfuko wa pili wa hatua kali za malipo ziliyotolewa na wakopeshaji. REUTERS/Yiannis Kourtoglou

Usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi wiki hii, Bunge la Ugiriki limepitisha mfuko awamu ya pili ya hatua zilizodaiwa na wakopeshaji. Mageuzi haya yanahusu sheria za kijamii na mabenki.

Matangazo ya kibiashara

Mageuzi haya ni sehemu ya masharti ya mwendelezo wa mazungumzo kwa ajili ya mpango wa tatu wa msaada.

Kwa kura 230 za ndio kwa jumla ya kura 300, serikali ya Alexis Tsipras ilibidi tena kutegemea sauti za upinzani za vyama vya Conservative (New Democracy), Kisoshalisti cha Pasok na chama cha mrengo wa kati cha To Potami.

Hata hivyo bado kuna mjadala mwingine wa haraka katika Bunge la Ugiriki. Wabunge wanatazamiwa kukutana kwa siku nzima ili kuzungumza nakala yenye kurasa zaidi ya mia moja waliyopewa Jumatatu ya juma hili. Katika hotuba yake kwa Bunge, Alexis Tsipras ina amerejelea kauli yake: " Serikali yangu haikubaliane na hatua ziliyopendekezwa na wakopeshaji ". Lakini amekumbusha kuwa hakua na njia nyingne: " Tuna maelewano magumu ili kuepuka mpango muhimu tulioombwa na nchi za Ulaya wa kukabiliana na hali hii inayoikumba nchi yetu. "

Upinzani pia ulifafanua msimamo wake. Chama cha Conservative cha New Demokrasy hakiungi mkono kura kwa ajili ya hatua za kukabiliana na mdororo wa kiuchumi au kura ya kuunga mkono serikali, lakini kura kuilinda Ugiriki katika Umoja Ulaya.

Wakati huo huo, wabunge 36 wamejiondoa katika mrengo wenye msimamo mkali wa kushoto wa Syriza kwa jumla ya wabunge 149 waliochaguliwa kwa tiketi ya chama cha Waziri mkuu. Kwa sasa imethibitika kuwa chama cha waziri mkuu na washirika wake vimegawanyika, licha ya kupitishwa kwa mfuko wa kwanza wa hatua wiki moja iliyopita. Wakati wakisubiri kupata ufumbuzi, serikali hiyo ina funguo za kuweza kuendelea kuzungumza. Sertikali ina matumaini ya kupata makubaliano kuhusu mpango wa msaada wa zaidi ya Euro bilioni 80 ifikapo Agosti 20.

Hatua zilizochukuliwa usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi wiki hii ni pamoja na kurekebisha sheria za kijamii ili kuongeza kasi mfumio wa vyombo vya sheria na sheria za Ulaya kuhusu muongozo wa mabenki.