UGIRIKI-ULAYA-UCHUMI

Ugiriki: mazungumzo juu ya mkopo mya wa kimataifa yaanza

Waziri mkuu Manuel Valls alionya dhidi ya "kugawanyika kwa Ulaya" Ugiriki itajiondoa katiaUmoja wa Ulaya, Julai 8, 2015 Bungeni.
Waziri mkuu Manuel Valls alionya dhidi ya "kugawanyika kwa Ulaya" Ugiriki itajiondoa katiaUmoja wa Ulaya, Julai 8, 2015 Bungeni. REUTERS/Jacky Naegelen

Mazungumzo kati ya serikali ya Ugiriki na wakopeshaji wake juu ya mpango wa tatu wa msaada yanaanza wiki hii katika mji mkuu wa Ugiriki, Athens. Ni mbio mpya zinazoanza katika suala hii.

Matangazo ya kibiashara

Ugiriki inakabiliwa na mzigo wa madeni na inatakiwa kulipa upya madeni yake mwishoni mwa mwezi Agosti.

Baada ya makubaliano ya Julai 13 kwenye mpango mpya wa msaada kwa Ugiriki wa karibu Euro bilioni 80 katika kipindi cha miaka mitatu, masharti na kalenda vitaendelea kujadiliwa kati ya Athens na wakopeshaji wakena majira kubaki kwa kuwa mazungumzo kati ya Ugiriki na wakopeshaji wake (nchi za Ulaya na IMF).

Mazungumzo yanaanza leo Jumatatu na katika mji wa Athens kama katika mji wa Brussels wana matumaini ya kukamilika kwa mazungumzo haya kabla ya Agosti 20, tarehe ambayo Ugiriki inatakiwa kulipa Benki Kuu ya Ulaya (ECB) Euro bilioni 3, na kisha, mwezi Septemba, Euro bilioni 1.5 kwa Shirika la fedha duniani (IMF).

Lakini bila msaada wa ziada wa mpango huu, Ugiriki itashindwa kukabiliana kulipa madeni hayo katika tarehe walizokubaliana na wakopeshaji wake. Serikali ya Ugiriki ametimiza sehemu ya makubaliano ya hatua kali za malipo yaliyopitishwa na Bunge, hatua ambazo liombwa na wakopeshaji wa Ugiriki. Wakopeshaji wa Ugiriki pia walikaribisha uamzi huo wa Ugiriki wa kupitisha hatua hizo.