Pata taarifa kuu
UFARANSA-MALAYSIA-UCHUNGUZI

Mabaki yanayokisiwa kuwa ya ndege ya MH370 yagunduliwa kisiwani Réunion

Wachunguzi wa Ufaransa wamejielekeza katika kisiwa cha Réunion kufanya uchunguzi kuhusu mabaki ya ndege yaliyogunduliwa kwenye pwani ya bahari Hindi.
Wachunguzi wa Ufaransa wamejielekeza katika kisiwa cha Réunion kufanya uchunguzi kuhusu mabaki ya ndege yaliyogunduliwa kwenye pwani ya bahari Hindi. Photo: Yannick Pitou/AFP
Ujumbe kutoka: RFI
2 Dakika

Wachunguzi wa Ufaransa wamejielekeza mapema Alhamisi wiki hii katika kisiwa cha Ufaransa cha Réunion katika Bahari ya Hindi, ili kuchunguza iwapo mabaki ya ndege yaliopatikana katika pwani ya kisiwa hicho ni ya Boeing 777 ya shirika la ndege la Malaysia Airlines.

Matangazo ya kibiashara

MH370 ya shirika la ndege la Malaysia Airlines ilipotea tangu Machi 8 mwaka 2014.

Mabaki yenye urefu wa mita mbili, yaligunduliwa na wafanyakazi wa shirika linalosafisha mifereji katika mji wa Saint-André katika kisiwa cha Reunion, kimebaini chanzo kilio karibu na kitengo cha uchunguzi wa kujua asili ya mabaki hayo.

" Inaonekana kuwa kifaa hikii kilikaa kwa muda mrefu katika maji ", wamesema mashahidi.

Hakuna dalili yoyote inayoonyesha mabaki hayo ni ya ndege gani, lakini wachunguzi wenye taaluma kutoka polisi ya Ufaransa wanachunguza hasa taarifa mbalimbali, kama vile namba ya kifaa hicho, ambayo itapelekea kutambuliwa kwa kifaa chenyewe.

Taarifa kutoka Marekani zimesema wachunguzi hao ambao wameona picha za mabaki hayo wana uhakika mkubwa kwamba ni ya ndege hiyo ya Malaysia ambapo mabaki hayo ni sehemu ya bawa la ndege.

Hata hivyo, Wataalamu wa Ufaransa wamesema ni mapema mno kutoa uhakika kwamba mabaki hayo ni lazima yatakuwa ya ndege ya Malaysia aina ya Boeing 777 ambayo kupotea kwake kumeleta gumzo la kidunia.

" Ni mapema mno kutoa uhakika kuhusu mabaki haya. Kwa sasa, inatubidi tuchunguze mabaki haya ni ya ndege gani. Wakati tutakua tumefanya jambo hili, hakuna shaka itatuwezesha kujua shirika la ndege linalomilikia ndege hii ", kimeeleza chanzo kilio karibu na uchunguzi.

Watu wapatao 239 waliokuwa wakisafiri na ndege hiyo walipoteza maisha.

Waziri wa Usafirishaji wa Malaysia Liow Tiong Lai akiwa ziarani mjini New York, Marekani, amesema nchi yake imetuma wataalamu zaidi kuchunguza mabaki hayo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.