UKRAINE-MAPIGANO-USALAMA

Ukraine: mapigano mapya wakati mazungumzo yakiendelea Minsk

Mapigano makali yameendelea kushuhudiwa katika maeneo ya magharibi ya ngome kuu ya waasi wanataka kujitnga kwa jimbo la Donetsk.
Mapigano makali yameendelea kushuhudiwa katika maeneo ya magharibi ya ngome kuu ya waasi wanataka kujitnga kwa jimbo la Donetsk. REUTERS/Alexander Ermochenko

Mapigano mapya yameibuka mashariki mwa Ukraine. Wanajeshi wanne wa Ukraine wameuawa ndani ya masaa 24 yaliopita, serikali ya Ukraine imetangaza Jumatatu ikibaini kwamba siku ya Jumapili "kulisuhudiwa hali ya machafuko". Donetsk, ngome kuu ya waasi, pamoja na bandari ya Mariupol ni maeneo yaliyoathirika zaidi.

Matangazo ya kibiashara

Mapigano haya yametokea mashariki mwa Ukraine kabla ya mazungumzo mapya mjini Minsk ya kujadili utekelezaji wa usitishwaji mapigano. Upande wa serikali, wametangaza kwamba wanajeshi wengi wameuawa na 15 wamejeruhiwa. Hii ni hasara kubwa zaidi ambayo imetangazwa na serikali ya Ukraine tangu majuma mawili yaliopita.

Kwa mujibu wa hesabu iliyotolewa na shirika la habari la Uingereza Reuters, karibu wanajeshi 30 Ukraine wameuawa na karibu 200 wamejeruhiwa mwezi wa Julai, licha ya kufikiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano mwezi Februari mwaka 2015. Vikosi vya serikali vimewatuhumu waasi wanaotaka kujitnga kwa eneo la mashariki mwa Ukraine kwamba wamekua wakitumia silaha nzito za kivita ziliopigwa marufuku na mkataba wa kusitisha mapigano.

Na hakika, mazungumzo hayo ya Minsk, yaliondaliwa katika " mpango wa kuwasiliana" chini ya mwamvuli wa Shirika la Usalama na Ushirikiano wa Ulaya, yana lengo la kuondoa silaha nzito za kivita kutoka mstari wa mbele wa mapigano.

Mahakama ya Katiba ya Kiev imeruhusu rasimu ya mageuzi ya kikatiba ambayo itapitishwa na Bunge. Mahakama hiyo inatoa uwezo kwa mabaraza ya wawakilishi wa mikoa na mitaa waliochaguliwa, lakini, kinyume na matarajio ya waasi wanaoungwa mkono na Urusi, haithibitishi kujitegemea kwa wilaya zilio chini ya udhibiti wa waasi hao.