UGIRIKI-ULAYA-UCHUMI

Ugiriki na wakopeshaji wake wasubiri mkataba wa moja kwa moja

Baada ya kuendelea mwishoni mwa wiki iliopita, mazungumzo kati ya Athens na wakopeshaji wake juu ya mpango wa tatu wa msaada kwa Ugiriki yameendelea kwa kasi Jumatatu wiki hii, kukiwa na matumaini ya kumaliza mazungumzo haraka iwezekanavyo, licha ya Ujerumani kujizuia.

Serikali ya Alexis Tsipras (kulia) imewasilisha mapendekezo yake mapya kwa Rais wa Ukanda wa nchi zinazotumia sarafu ya Euro Jeroen Dijsselbloem (kushoto) saa mbili kabla ya tarehe ya mwisho iliyopangwa kutamatika.
Serikali ya Alexis Tsipras (kulia) imewasilisha mapendekezo yake mapya kwa Rais wa Ukanda wa nchi zinazotumia sarafu ya Euro Jeroen Dijsselbloem (kushoto) saa mbili kabla ya tarehe ya mwisho iliyopangwa kutamatika. REUTERS/Petros Giannakouris/Pool
Matangazo ya kibiashara

Kwa siku nzima, Ugiriki imeendelea na mazungumzo katika na wakopeshaji wake, Umoja wa Ulaya, benki kuu ya Ulaya (BCE), Shirika la Fedha Duniani (IMF) na taasisi ya kukabiliana na mdororo wa kiuchuni barani Ulaya (ESM). Mazungumzo hayo yamefanyika katika hoteli katika kituo cha Athens.

Mpaka sasa Ugiriki imetakiwa kutoa ahadi yenye nia njema kwa kukubali mageuzi mazuri ya uchumi wa nchi, ili iweze kupewa msaada wa Euro bilioni 80 kwa miaka mitatu mfululizo, kiasi cha pesa bado hakijafahamika.

Mazungumzo yamerejelewa Jumatatu asubuhi wiki hii, chanzo cha serikali kimeliambia shirika la habari la Ufaransa (AFP), huku chanzo hicho kikisem akuwa mazungumzo hayo yamerejelewa " kwa kasi, lakini bila machafuko ".

Jumatau subuhi wiki hii, baadhi wamekua na matumaini ya makubaliano Jumanne wiki hii au kuanzia Jumatatu usiku kwa wale wenye matumaini ya karibu.

Annika Breidthardt, msemaji wa Tume ya Ulaya, amesema kuwa " taasisi (wakopeshaji) zinafanya kazi bega kwa bega na viongozi wa Ugiriki."

" Kuna maendeleo makubwa na tuna matumaini ya mengine wakati wa mchana, wakati ambapo mazungumzo yanaendelea kuhusu suala ambalo bado halijapatiwa suluhu ", ameongeza Annika Breidthardt.