UTURUKI-SYRIA-USALAMA

Wanajeshi wa Uturuki waonekana Syria

Mwanamgambo wa Turkmen katika mji wa Aleppo mwezi Januari mwaka 2013.
Mwanamgambo wa Turkmen katika mji wa Aleppo mwezi Januari mwaka 2013. AFP PHOTO/JM LOPEZ

Hata kama serikali ya Uturuki imeendelea kukanusha, lakini taarifa zinasema kuwa hadi wanajeshi 600 wa Uturuki wamejiunga na wapiganaji wa Uturuki kutoka jamii ya  Turkmen na kupelekwa Kaskazini mwa Syria tangu Jumatatu usiku.  

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa wanamgambo wa Turkmen, kundi lililoundwa hivi karibuni chini ya ufadhili wa Ankara, amethibitisha kuwepo kwa wanajeshi 600 wa Uturuki nchini Syria. Waziri Mkuu wa Uturuki, Ahmet Davutoglu, pia alizungumzia jana katika mahojiano ya televisheni, uwezekano wa kupeleka wanajeshi wa nchi kavu ili kujihami.

Uwepo wa wanajeshi au maafisa wa Idara ya Ujasusi ya Uturuki umeelezwa na mashahidi tafauti kwenye eneo hilo, ikiwa ni pamoja na wanakijiji, waandishi wa habari na viongozi wa Kikurdi, amearifu mwandishi wetu mjini Istanbul, Jerome Bastion. RFI imepata taarifa hii kutoka kwa mpiganaji wa kundi la kiislam lenye silaha Ahrar-ul-Sham, mshirika wa Ankara. Mwenyewe kutoka kikabila la Turkmen, yuko kwenye mpaka walikopita Jumatatu wapiganaji kutoka kundi la wanamgambo wa Turkmen wakiingia Syria.

Ushiriki wa Uturuki kwa kundi hili la wanamgambo, kundi lililoanzishwa kwa siri nchini Uturuki wiki mbili zilizopita, inaelezwa, ikiwa tu kwa msaada ambao Uturuki inaweza kulipatishia kwa kutumia vifaa na silaha ambavyo lililetewa. Vifaru na vifaa vya kijeshi, ni sehemu ya msaada kundi hili lilipatishiwa. Uwepo wa wanamgambo wa Turkmen kwenye mpaka wa Uturuki na Syria ni dhahiri kuwa ni washirika asilia wa Uturuki, kwa sababu wanaongea Kituruki na wameomba kwa muda mrefu msaada kutoka serikali ya Ankara.

Deni la kihistoria

Msaada huu, unaowasilishwa kama deni la kihistoria kutokana na kizazi cha Ottoman, ulitetewa mwaka jana na viongozi wa Uturuki wakati shehena ya silaha ziliokua zikipelekwa Syria kukamatwa. Hadi wakati huo wanamgambo hao kutoka kabila la Turkmen waliunda makundi ya ya kujihami, lakini wakati huu, wamekua washirika wa karibu wa serikali ya Ankar kwa kulinda eneo lenye ulinzi kati ya Aleppo na mpakani, ili kuimarisha vikundi vya waasi wenye msimamo wa wastani na kuwaweka mbali Wakurdi.