Pata taarifa kuu
UGIRIKI-ULAYA-UCHUMI

Ugiriki: Bunge lapasisha makubaliano yaliyofikiwa kwa mpango wa 3 wa msaada

Waziri Mkuu Alexis Tsipras (kulia) anapaswa kulishawishi Bunge la Ugiriki ili lipigie kupiga kura Alhamisi jioni, muongozo wa nchi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Waziri Mkuu Alexis Tsipras (kulia) anapaswa kulishawishi Bunge la Ugiriki ili lipigie kupiga kura Alhamisi jioni, muongozo wa nchi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo. REUTERS/Alkis Konstantinidis
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Wabunge nchini Ugiriki wamepiga kura nchi hiyo ikubaliane na masharti ya mpango wa tatu wa kimataifa kuhusu kusaidiwa mkopo, mpango ambao mpaka sasa umeligawa taifa hilo.

Matangazo ya kibiashara

Kura hii imeanyika wakati ambapo mawaziri wa fedha kutoka Umoja wa Ulaya wakitarajiwa kuketi baadae hii leo Ijumaa kutoa uamuzi wao kuhusu mapendekezo mapya yaliyokubaliwa na utawala wa Athens pamoja na wakopeshaji baada ya miezi kadhaa ya majadiliano.

Mawaziri hawa wanakutana huku nchi ya Ujerumani yenyewe ikiwa bado haijaamua iwapo iidhinishe mapendekezo hayo mapya ya Ugiriki au la, kwa kile viongozi wa Berlin wanasema kuwa, wanataka kwanza wapate maelezo ya kina kuhusu mpango huu.

Iwapo wabunge watakataa masharti mengine ya wakopeshaji wa kimataifa, huenda kukasababisha nchi hiyo kuhitaji msaada zaidi wa fedha za dharura kuinusuru Serikali kushindwa kujiendesha.

Nchi ya Finland imekuwa taifa la kwanza kuidhinisha mapendekezo ya Ugiriki na kutoa masharti zaidi kwa nchi hiyo wakati huu ikijaribu kuhakikisha inapatiwa kiasi cha dola za Marekani bilioni 94.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.