UGIRIKI-MAKEDONIA-WAHAMIAJI-USALAMA

Wahamiaji wavuka kwa nguvu mpaka wa Ugiriki na Makedonia

Wahamiaji walivuka mpakakwa nguvu wakiingia Makedonia, Jumamosi, Agosti 22, 2015. Walijielekeza kwenye cha treni cha Gevgelija ambapo kunapatikana treni zinazosafiri kwenda mpakani na Serbia.
Wahamiaji walivuka mpakakwa nguvu wakiingia Makedonia, Jumamosi, Agosti 22, 2015. Walijielekeza kwenye cha treni cha Gevgelija ambapo kunapatikana treni zinazosafiri kwenda mpakani na Serbia. REUTERS/Ognen Teofilovski

Jumamosi mchana, Agosti 22, mamia ya wahamiaji walipenya na kuingia kwa nguvu kusini mwa Makedonia huku wakikabiliana na polisi ambayo baadaye ilizidiwa nguvu. Kisha mapema jioni, wakimbizi wengine 1,500 waliweza kuvuka mpaka na kuingia Makedonia.

Matangazo ya kibiashara

Wakimbizi hao ni pamoja na raia wa Syria, ambao baada ya kupitia Ugiriki, walitaka kusafiri kwenda Ulaya Magharibi, wakipitia Makedonia, Serbia na Hungary.

Kutokana na na kuwasili kwa wahamiaji wengi nchini mwake wakitokea Ugiriki, serikali ya Makedonia ilitangaza Alhamisi wiki hii hali ya hatari kwa kukabiliana na ongezeko hili la wakimbizi. Jeshi na vikosi maalum vya polisi vimepelekwa eneo la mpaka. Tangu wakati huo, watu zaidi ya elfu mbili walikusanyika katika eneo hilo la mpaka, wakilala usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi katika mazingira magumu, huku mvua nyingi zikinyesha.

Wakimbizi mia kadhaa, wengi wao wakiwa wenye asili ya Syria ambao walikua walikata tamaa, waliweza kuvuka vizuizi Jumamosi Agosti 22, wakikabiliana na polisi ambayo imekua ikirusha mabomu ya kuwatawanya. Makabiliano hayo yalidumu dakika chache tu lakini hali bado ni nzito. hali ambayo huenda ikalipuka hivi karibuni katika nchi za Ulaya, ambazo zimeshindwa na sera ya uhamiaji, amearifu mwandishi wetu katika mji wa Athens, Alexia Kefalas.

Kufuatia milipuko huo, wahamiaji walijielekeza katika kituo cha treni cha Gevgelija, ambapo kunapatikana treni zinazosafiri kwenda mpakani na Serbia. Katika kituo hicho cha treni, wahamiaji hao walijiunga na baadhi ya wahamiaji wengine elfu mbili ambao walikua tayari kujielekeza barani Ulaya. Wakimbizi wote hao wanapanga kwenda Ujerumani wakipitia Hungary.

Itafahamika kwamba Hungary imeanza ujenzi wa uzio wa mita nne kwenda juu kwenye mpaka wake ili kuzuia wahamiaji kuvuka na kuingia nchini humo.

Hatimaye, mapema Jumamosi jioni, baadhi ya wahamiaji 1500 waliweza kuingia, bila makabiliano yoyote na polisi nchini Makedonia (jamhuri ya zamani ya Yugoslavia) na kuvuka hatua moja zaidi katika safari yao ya Ulaya Magharibi.