CHINA-UINGEREZA-UFARANSA-UJEUMANI-HISA-UCHUMI

Mgogoro wa uchumi China waathiri mataifa ya Ulaya

Biashara katika Masoko ya hisa jijini London, Paris na Frankfurt imeshuka kutokana na mgogoro wa uchumi unaoendelea kushuhudiwa nchini China.

Watembea kwa miguu watupia macho kwenye ubao wa kibiashara mjini Tokyo, Agosti 24, 2015.
Watembea kwa miguu watupia macho kwenye ubao wa kibiashara mjini Tokyo, Agosti 24, 2015. Photo par YOSHIKAZU TSUNO/AFP
Matangazo ya kibiashara

Hali hii imewapa wasiwasi wafanyabishara nchini China na katika mataifa mengine ya Ulaya kutokana na kuyumba kwa uchumi wa China na pia mtikisiko katika soko lake la hisa.

Hali ya masoko ya hisa nchini China yamekuwa yakiyumba toka mwezi Juni mwaka huu na siku ya Jumatatu masoko mengi barani Ulaya yamefunguliwa huku hisa zikiwa chini.

Wawekezaji wa Kimataifa wameanza kuhofia hali ya kiuchumi nchini China ambayo ni ya pili duniani baada ya Marekani ikiwa hali hii itaendelea kushuhudiwa katika siku zijazo.

Wiki mbili zilizopita, Benki kuu nchini humo ilipunguza thamani ya sarafu ya Yuan ikilinganishwa na sarafu ya Dola.

Wachumi wanasema sababu kubwa inayoifanya China kupitia hali hii ni kwa sababu ya kununua idadi kubwa ya bidhaa nje ya nchi badala ya kuuza.