UGIRIKI-MAKEDONIA-WAHAMIAJI-USALAMA

Wahamiaji wafanya safari ndefu kwa kwenda Ulaya Magharibi

Makedonia imeachana na uamzi wa kuwazuia wahamiaji. Tangu wiki hii, wahamiaji wanaweza kuingia nchini humo bila hofu yoyote ya kukamatwa.

Wahamiaji wanasubiri treni katika kituo cha reli cha Gevgelija, ncini Makedonia, Agosti 15, 2015.
Wahamiaji wanasubiri treni katika kituo cha reli cha Gevgelija, ncini Makedonia, Agosti 15, 2015. REUTERS/Stoyan Nenov
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huo unsaidia kupunguza ghasia wakati ambapo polisi ya Makedonia ilitumia mabomu ya machozi dhidi ya maelfu ya wahamiaji wiki iliyopita. Hali kwa sasa ni tulivu kwenye barabara ya reli mbapo wahamiaji hao hupita kwa kwenda Ulaya Magharibi wakipitia Serbia.

Mara kadhaa kwa siku, wahamiaji wanapaswa kuamka na kutoa njia kwa treni. Kisha wanavuka mpaka wa Ugiriki na Makedonia kwa vikundi vya watu 50, jeshi na polisi vikishuhudia, amearifu mwandishi wetu katika mji wa Gevgelija, Charlotte Stiévenard.

George aliwasili karibu saa sita mchana. Raia huyu kutoka Syria ana imani kuwa hali kwa sasa ni tulivu, hata kama hata kama wamekua wakisubiri kwa muda mrefu: "Hakuna hali yoyoyte ya wasiwasi, ikilinganishwa na yale tuliona kwenye televisheni siku chache zilizopita. Wasiwasi wangu tu ni kwamba tuna safiri usiku, lakini haitakua usiku wangu wa kwanza kusafiri kwa mguu porini, lakini hata hivyo itakuwa vigumu sana ", amesema George.

Tangu Machi, Madaktari wasio na mipaka hutoa misaada kwa wahamiaji ambao wamekua wakielekea Ulaya Magharibi. Stathis Kyroussis ni mkuu wa ujumbe wa mashirika yasiyo ya kiserikali. Kwa upande wake, amesema kuzuia mpaka huleta matatizo.

Siku hiyo, Stathis Kyroussis alihesabiwa watu 1 500. Mara baada ya kuvuka mpaka, wahamiaji hao walisajiliwa na polisi ya Makedonia na waliendelea na safari yao nchini Serbia wakielekea Ulaya ya Kaskazini.

■ Bulgaria yapeleka askari mpakani

Tangu mwanzoni mwa mwaka, Bulgaria imewapokea wahamiaji haramu 15 000, ikiwa ni pamoja na raia wa Syria. Tayari ukuta umejengwa kwenye mpaka wake na Uturuki. Kutokana na wingi wa wahamiaji kutoka Makedonia, katika siku za karibuni, Sofia aliamua Jumanne Agosti 25, kupeleka wanajeshi kwenye mpaka wake ili kuhakikisha usalama.