Pata taarifa kuu
UGIRIKI-UCHAGUZI-SIASA

Tsipras awasihi raia wa Ugiriki

Alexis Tsipras mbele ya Bunge la Ugiriki Jumamosi Julai 11. Bunge linatakiwa kupitisha mpango wa kwanza wa mageuzi kabla ya Alhamisi Julai 16.
Alexis Tsipras mbele ya Bunge la Ugiriki Jumamosi Julai 11. Bunge linatakiwa kupitisha mpango wa kwanza wa mageuzi kabla ya Alhamisi Julai 16. REUTERS/Alkis Konstantinidis
Ujumbe kutoka: RFI
2 Dakika

Kiongozi wa mrengo wa kushoto nchini Ugiriki, Alexis Tsipras Jumapili hii, alitoa wito kwa wapiga kura kumpa " mamlaka yenye nguvu, wingi wa viti " katika uchaguzi wa wabunge wa Septemba 20 mwaka 2015, lengo ambalo linaonekana ni ndoto kwa Waziri mkuu wa zamani licha ya chama cha Syriza kuongoza katika utafiti wa kabla ya uchaguzi huo.

Matangazo ya kibiashara

Katika mahojiano na gazeti la kila wiki la Realnews juu ya suala la uchaguzi huu wa wabunge utakaofanyika wiki tatu zijazo, Alexis Tsipras, ambaye anawania awamu ya pili, ameonyesha dhamira yake: " Ni rahisi, wazi na wenye misingi ya kidemokrasia: tunahitaji mamlaka yenye nguvu , wingi wa viti kwa serikali ya chama cha Syriza " kwa kipindi cha miaka minne ijayo.

Na kuongeza kuwa: " Hii ni nafasi ya kuondokana na vyama viwili ikiwa ni pamoja na New Democracy (ND, kulia) na PASOK (chama cha kisoshalisti)," vyama viwili ambavyo vilitawala siasa za Ugiriki kwa kipindi cha miaka arobaini iliopita (... ). Ni muhimu kwa kutorudi nyuma na kupiga hatua mbele. "

Kikiongoza kutoka pointi 1 hadi 3.5, kwa mujibu wa utafiti wa taasisi ya Ugiriki, dhidi ya chama cha upinzani cha New Democracy (ND), chama cha Syriza kina nafasi ndogo ya kupata wingi wa viti wakati wa uchaguzi huo.Alexis Tsipras atalazimika kutafuta washirika kwa kuunda serikali ya umoja kama alivyofanya baada ya ushindi wake Januari 25, ambapo alishindwa kupata wingi wa viti.

Utafiti mmoja pekee uliofanywa na na shirika liitwalo Think tank Bridging Europe, inatoa mpaka sasa fursa ya wazi ya pointi nane kwa chama cha Syriza (26.8%) dhidi ya chama cha New democracy (ND).

- "Mfumo wa zamani" -

Alexis Tsipras tayari amefutilia mbali muungano wowote na vyama vyenye, " mfumo wa zamani wa kisiasa", akisisitiza kuwa chama peke cha Anel, mshirika wakew katika serikali kwa miezi nane, kinaweza kushirikishwa katika serikali ya umoja.

Kwa upande mwingine, vyama vya ND, PASOK na To Potami (katikati kushoto) vimesema viko tayari kushirikiana na wengine.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.