ULAYA-WAHAMIAJI-USALAMA

Ulaya kutathmini kuhusu ongezeko la wahamiaji

Viongozi kadhaa wa Ulaya wamesimama kidete Jumapili Agosti 30 kuhusu haki ya ukimbizi kwa wakimbizi wanaoingia kwa wingi barani Ulaya.

Kundi la wahamiaji wakiingia katika treni katika mji wa Gevgelija, Makedonia, Agosti 29, 2015 baada ya kuvuka mpaka wa Ugiriki.
Kundi la wahamiaji wakiingia katika treni katika mji wa Gevgelija, Makedonia, Agosti 29, 2015 baada ya kuvuka mpaka wa Ugiriki. Photo par ARIS MESSINIS/AFP
Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati wahamiaji wamekua wakiendelea kuvuka kwa mamia, mpaka wa serbia na Hungary, moja ya milango ya kuingilia ya Umoja wa Ulaya, licha ya kukamilika kwa uzio wa nyaya wenye lengo la kuzuia wahamiaji hao kuendelea kuingia Ulaya.

Waziri Mkuu wa Ufaransa na mawaziri wa mambo ya nje wa Italia na Ufaransa wametetea msimamo wao kwa hatua ya haraka ya kuwapa hifadhi wakimbizi, wakati Berlin, London na Paris wametoa wito wa mkutano wa mawaziri katika wiki mbili zijazo " kupiga hatua madhubuti " juu ya mgogoro wa suala la uhamiaji.

Katika taarifa ya pamoja, mawaziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa, Ujerumani na Uingereza ambo ni Bernard Cazeneuve, Thomas de Maiziere na Theresa May, wamekumbusha ikiwa ni pamoja na " uharaka wa kuanzisha, kabla ya mwisho wa mwaka huu nchini Ugiriki na Italia " zoezi la haraka, la kuchagua vituo kwa ajili ya kubainisha kati ya watu wanaoweza kupata haki ya ukimbizi na wahamiaji haramu wa kiuchumi.

Mawaziri hao watatu pia wametaka kuanzishwe, " haraka sana ", "orodha ya nchi za uhakika wanakotokea watu hao " ili kuweza kujaza faili ya hifadhi ya pamoja kwa Ulaya, kuwalinda wakimbizi na kuhakikisha ufanisi wa kuwarejesha wahamiaji haramu katika nchi zao ".

" Italia imepania kuanzisha mapambano katika miezi ijayo juu ya kupatikana kwa haki ya hifadhi barani Ulaya ", amesema Jumapili hii Waziri Mkuu Matteo Renzi.