UHOLANZI-HUNGARY-UFARANSA-WAKIMBIZI-USALAMA

Uholanzi yajiandaa kulegeza sheria juu ya hifadhi kwa wakimbizi

Uholanzi inajiandaa kulegeza sheria juu ya hifadhi kwa wakimbizi. Serikali imepania kufuta misaada ya chakula na hifadhi kwa wakimbizi ambao maombi yao yalikataliwa. Raia hao wakigeni watakua tu na wiki chache kuondoka nchini humo.

Watu wanaotafuta hifadhi, kusini magharibi mwa Uholanzi, huchukuliwa na kupelekwa kwenye nafasi iliyotayarishwa na shirika la kuchunguza kesi zao, Julai 20, 2015.
Watu wanaotafuta hifadhi, kusini magharibi mwa Uholanzi, huchukuliwa na kupelekwa kwenye nafasi iliyotayarishwa na shirika la kuchunguza kesi zao, Julai 20, 2015. AFP PHOTO / ANP / ARIE KIEVIT
Matangazo ya kibiashara

Vituo thelathini vya mapokezi katika mikoa mbalimbali vitafungwa, vituo vya kitaifa sita vitaendelea kufanya kazi hususan kuwapokea raia wa kigeni ambao watakubali kurejea katika nchi zao walikotoka. Serikali ya Uholanzi imesema tatizo si kwa wanaotafuta hifadhi ambao faili zao zinafanyiwa uchunguzi, na kwa wale ambao ombi maombi yao yalikubaliwa, lakini kwa watu wengi ambao wamekua wakikataa kuondoka nchini Uholanzi, wakati ambapo walinyimwa hadhi ya ukimbizi chini ya Umoja wa Mataifa, na walipewa taarifa kuhusu hati ya kunyimwa hifadhi hiyo.

Nchi ya Hungury, kwa upande wake, imetupilia mbali matamshi ya waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Laurent Fabius, ambaye mwishoni mwa juma alikosoa namna ambavyo nchi hiyo inashughulikia tatizo la wahamiaji haramu wanaoingia Ulaya kupitia nchini humo.

Kwenye mahojiano maalumu na kituo kimoja cha Redio cha Ufaransa, waziri Fabius amesema kuwa anashangaa kuona baadhi ya nchi zikikataa kuwapokea wahamiaji huku nyingine zikifikia hata hatua ya juu kabisa ya kuweka ukuta maalumu kuwazuia wahamiaji na hata kuwafunga.

Matamshi haya ya waziri Fabius, anayatoa wakati huu ambapo wakuu wa nchi za Uingereza na Ufaransa wameitisha mkutano wa dharura wa nchi wanachama za Umoja wa Ulaya, ndani ya majuma mawili yajayo, kujadili suala la wahamiaji.