UFARANSA-USALAMA-UCHUMI

Mkutano wa Hollande na vyombo vya habari: Syria, wahamiaji na kupunguza kodi

Rais wa Ufaransa, François Hollande, wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari, Septemba 7, 2015.
Rais wa Ufaransa, François Hollande, wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari, Septemba 7, 2015. REUTERS/Charles Platiau

Katika mkutano wake mkuu wa sita na vyombo vya habari Jumatatu wiki hii, Rais wa Ufaransa François Hollande ameungumzia kuhusu mashambulizi dhidi ya Kundi la Islamic State nchini Syria.

Matangazo ya kibiashara

Rais Hollande pia amezungumzia mapokezi ya wakimbizi na maelezo ya kina yanayosubiriwa kuhusu punguzo la kodi iliyopangwa mwaka 2016.

Kwa mujibu wa mkutano huo wa kawaida wa kila baada ya miezi sita uliofanyika Jumatatu mchana wiki hii, mkutano ambao wameshiriki zaidi ya waandishi wa habari 200 katika Ikulu ya Elysée, na mkutano huu umerushwa moja kwa moja hewani kwenye runinga ya France 2 na vyombo vingine vya habari. François Hollande ameendesha mkutano huo kwa muda wa masaa mawili.

Rais wa Ufaransa amezungumzia kuhusu mashambulizi ya anga dhidi ya kundi la Daech (IS), wakati ambapo tishio la kigaidi bado ni kubwa nchini Ufaransa, kama ilivyoshuhudiwa katika shambulio lililotekelezwa Agosti 21 katika treni ya mwendo wa kasi iliyokua ikisafiri kutoka Amsterdam kwenda Paris (Thalys).

Rais, ambaye alikutana siku ya Ijumaa na bodi ndogo ya upande wa ulinzi, anatarajia msaada wa vigogo wa nchi, ambao wameendelea mwishoni mwa wiki hii kutoa taarifa mbalimbali zinazounga mkono suala hili.

Suala la mapokezi ya wakimbizi limepewa kipaumbele katika hotuba hiyo ya rais. Wakati huo rais Hollande ameeleza bayana kwamba Ufaransa iko tayari "kuwapokea wakimbizi", hasa wale wanaokimbia kutoka Syria.

Alhamisi wiki iliyopita, Berlin na Paris walizindua mpango kwa "kuandaa mapokezi ya wakimbizi na mgawanyo ulio sawa kati ya nchi za Ulaya."

Suala la punguzo la kodi

Rais Hollande amefafanua uzito na taratibu kuhusu suala la punguzo la kodi ambalo alitangaza Agosti 21 kwa mwaka 2016, wakati ambapo miaka yake mitano imebaki kwenye mstari mwekundu.