Pata taarifa kuu
UTURUKI-IS-PKK-MSHAMBULIZI-USALAMA

Uturuki: Ndege za kijeshi zaendesha mashambulizi dhidi ya waasi wa PKK

Wanakijiji wakitafuta miili ya askari waliouawa katika mashambulizi ya Septemba 7, 2015 katika mji wa Daglica,  kusini mwa Uturuki.
Wanakijiji wakitafuta miili ya askari waliouawa katika mashambulizi ya Septemba 7, 2015 katika mji wa Daglica, kusini mwa Uturuki. AFP/DICLE NEWS AGENCY/AFP

Ndege za kijeshi za Uturuki zimeendesha mashambulizi ya anga usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne wiki hii dhidi ya ngome kuu za waasi wa PKK, kaskazini mwa Iraq, kwa kujibu shambulizi lililowaua wanajeshi wake 16, limetangaza shirika la habari la serikali.

Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya ndege 50 za kijeshi zimeendesha mashambulizi kwa muda wa masaa sita dhidi ya maeneo 20 ya waasi wa kikurdi wa PKK, na kuua kati ya “magadidi 35 na 40”, limethibitisha shirika hilo la habari la serikali.

Makambi ya Qandil, Hakurk, Zap, Metina, Gare na Basyan zililengwa na mashambulizi hayo, shirika hilo la habari limearifu.

Kundi la magaidi kati ya 20 na 25 ni miongoni mwa vitu vtu viliyoshambuliwa na ndege za kijeshi la Uturuki. Magaidi hao walikua wakikimbia kutoka Uturuki wakirejea katika makambi yao, kwa mujibu wa shirika hilo la habari la serikali nchini Uturuki.

Operesheni hiyo inakuja baada ya shambulio lililosababisha vifo vya askari 16 Jumapili katika mji wa Deglica, Kaskazini mwa Uturuki, kwenye mpaka na Iraq.

Serikali ya Uturuki iliahidi Jumatatu wiki hii kulitokomeza kundi la waasi wa PKK, siku moja baada ya shambulio hilo baya kabisa lililoendeshwa shidi ya vikosi vya jeshi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.