MAREKANI-UINGEREZA-AJALI

USA: Ajali ya moto yatokea katika ndege ya British Airways

Maafisa wa zima moto wakikizima moto katika ndege ya British Airways, Septemba 8, 2015 katika uwanja wa ndege wa McCarran katika mji wa Las Vegas.
Maafisa wa zima moto wakikizima moto katika ndege ya British Airways, Septemba 8, 2015 katika uwanja wa ndege wa McCarran katika mji wa Las Vegas. AFP/AFP

Ndege ya shirika la British Airways imewaka moto wakati ilikua ikijianda kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Las Vegas, nchini Marekani, Jumanne wiki hii. Watu 172 waliokua katika ndege hiyo wameokolewa kwa dharura, ikiwa ni pamoja na watu saba ambao wamepata majeraha madogo.

Matangazo ya kibiashara

Abiria 159 na wafanyakazi 13 wa ndege hiyo, ikiwa ni pamoja na marubani watatu pamoja na wafanyakazi wengine kumi, kwa mujibu wa shirika la British Airways ndio waliokua katika ndege hiyo.

Kwa mujibu wa akaunti ya Twitter ya mamlaka ya uwanja wa ndege wa McCarran, watu saba miongoni mwa watu waliokua katika ndege hiyo wamepata majeraha madogo.

Runinga nyingi za Las Vegas zimearifu kuwa watu 14 ndio wamelazwa hosptalini kutokana na majerha madogo walioyapata, zikiwanukuu afisa wa kuzima moto wa kaunti ya Clark, katika mji wa Nevada, ambako kunapatikana uwanja wa ndege wa Las Vegas (Magharibi mwa Marekani)

Katika taarifa yake, British Airways kwa upande wake imeeleza " idadi ndogo ya wateja na wafanyakazi ambao wamepelekwa hospitalini kwa tahadhari ".

Katika rekodi ya cockpit iliyorushwa hewani kwenye mtandao na kwenye runinga za Marekani, kumesikika sauti ya dereva akitoa wito kwa ajili ya msaada: "SOS SOS Tunahitaji afisa wa zima moto ".

Kwa mujibu wa mamlaka ya safari za ndege (FAA), tukio hilo limetokea wakati " injini ya kuhoto ya Boeing 777-200 ya British Airways iliwaka moto wakati wa ikijiandaa kuruka ", kwenda kwenye uwanja wa ndegea wa Gatwick, mjini London, nchini Uingereza.