Pata taarifa kuu
UTURUKI-MACHAFUKO-USALAMA

Uturuki yakabiliwa na ongezeko la machafuko

Waandamanaji nchini Uturuki mbele ya majengo ya gazeti la "Hurriyet", linalotuhumiwa kuikosoa serikali, Jumanne Septemba 8.
Waandamanaji nchini Uturuki mbele ya majengo ya gazeti la "Hurriyet", linalotuhumiwa kuikosoa serikali, Jumanne Septemba 8. REUTERS/Murat Saka

Baada ya mashambulizi yaliyosababisha vifo vya watu wengi Kusini Mashariki mwa Uturuki, machafuko yameanza kujitokeza kati ya raia.

Matangazo ya kibiashara

Wakati wa maandamano yaliyokumbwa na vurugu, wafuasi wa caham tawala wamevamia na kushambulia majengo ya HDP, chama kikuu chenye wafuasi wengi kutoka jamii ya Wakurdi, na yale ya gazeti la Hürriyet, ambalo linatuhumiwa kuikosoa serikali. Hatua ya kutotoka nje imetangazwa katika miji kadhaa.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI katika mji mji wa Istanbul, Jérôme Bastion, Uturuki inakabiliwa ongezeko la machafuko ambayo yamesamba hadi kwa raia wa kawaida. Jumapili mwishoni mwa wiki iliyopita, mashambulizi yanayodaiwa kutekelezwa na wapiganaji wa Kikurdi wa kundi la PKK yaliwaua watu 16 katika safu ya jeshi la Uturuki, hali ambayo ilipelekea jeshi kulipiza kisase. Na Jumanne asubuhi wiki hii, askari polisi 14 wa Uturuki waliuawa kwa risasi, mauaji ambayo yalidaiwa kutekelezwa na kundi la raia wa Uturuki wanaotaka kujitenga.

Katika mji wa Ankara, chini ya kisingizio cha kuandamana " dhidi ya ugaidi wa PKK ", waandamanaji kadhaa wa Kiislam kutoka chama madarakani walivamia na kushambulia usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano wiki hii majengo ya chama kikuu chenye wafuasi wengi kutoka jamii ya Wakurdi cha HDP. Na kwa mara ya pili mfululizo usiku wa Jumanne majengo ya gazeti la Hürriyet, linalotuhumiwa kukosoa sera za serikali yalishambuliwa kwa mawe na wafuasi wa chama cha AKP cha Recep Tayyip Erdogan.

Hata hivyo polisi inatuhumiwa kuegemea upande wa serikali na chama madarakani na kutojali mashambulizi yanayoendeshwa dhidi ya majengo ya chama chenye wafuasi wengi kutoka jamii ya Wakurdi cha HDP, majengo ambayo mengi, ikiwa ni pamoja na makao makuu katika mji wa Ankara yalichomwa moto. Majengo ya vyama vya HDP, DBP, na wakati mwingine yale ya CHP yaliharibiwa katika miji kadhaa. Wimbi la ghasia ambalo Mbunge wa upinzani amelitaja kuwa la hatari linalochochewa na utawala wa Erdogan.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.